BM BARBERSHOP KINONDONI

Tuesday, August 21, 2012

BREAKING NEWS!!!!!!!!!! MAHAKAMA KUU KANDA YA TABORA YAMVUA UBUNGE DR. KAFUMU IGUNGA


BREAKING NEWS!!!!!!!!!! MAHAKAMA KUU KANDA YA TABORA YAMVUA UBUNGE DR. KAFUMU IGUNGA
Pichani ni aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Igunga Mh. Dk. Dalaly Peter Kafumu (mwenye skafu) akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama (mwenye miwani). (Picha na Maktaba)
Hukumu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na Wakazi wa Jimbo la Igunga imetolewa leo na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora ambapo imemuengua mbunge wa Jimbo hilo kupitia tiketi ya CCM Dk. Dalaly Peter Kafumu. Hukumu hiyo imetolewa kufuatia kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa akigombania nafasi hiyo ya Ubunge kupitia chama cha CHADEMA Joseph Kashindye. Hukumu hiyo inaendeleza wimbi la chama tawala CCM kupoteza majimbona kuweka alama katika Demokrasia ya Tanzania huku Wananchi wakijiuliza tunatoka wapi tunakwenda wapi.
 
HABARI KAMILI
Kwa hukumu hiyo sasa, Jimbo la Igunga mkoani Tabora liko wazi kuanzia leo baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kumvua ubunge Dr. Peter Dalay Kafumu wa CCM kufuatia hukumu iliyotolewa leo katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliomuweka madarakani mbunge huyo ambayo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Kashindye.

Taarifa kutoka Tabora zimeeleza kuwa hukumu hiyo iliyovuta hisia za maelfu ya wakazi wa mji huo na maeneo ya jirani, ilisomwa kuanzia mishale ya saa 3:00 asubuhi. Pamoja na Kafumu, Kashindye pia aliwashitaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Protace Mgayane . Shauri hilo lilianza kusikilizwa na Jaji Mary Nsimbo Shangali tangu Machi 26, 2012.

Akizungumza baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Dr. Kafumu amesema kuwa hajaridhishwa na hukumu pamoja na mwenendo mzima wa kesi hiyo kwani yeye alichofanya wakati wote wa kampeni ilikuwa ni kunadi sera za chama chake (CCM). Kafumu aliongeza vile vile kuwa tangu awali, alishaeleza mara kadhaa kuwa haridhishwi na jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo kwa vile alikuwa akiegemea upande mmoja; na kwamba ndicho alichokifanya leo wakati akitoa hukumu.

Kafumu ambaye kabla ya kujitosa kwenye siasa alikuwa ni Kamishna wa Madini, alisema kuwa uamuzi wote kuhusu nini cha kufanya baada ya uamuzi wa mahakama leo anauacha kwa chama chake (CCM) na kwamba hivi sasa, yeye atarejea katika kazi yake ya utaalam wa madini. Awali, Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Nzega, Sylvester Kainda, alikaririwa akisema kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora ilipanga hukumu hiyo isomwe jana lakini kutokana na siku hiyo kuwa Idd Pili, hukumu ikasomwa leo.

2 comments:

  1. Aisee! Sasa hii inadhihirisha CDm sio chama cha kuchezea na kwamba enzi zile za kuwafumba macho wananchi kwa kupindisha utaratibu kwa sababu ya kuwepo vyama dhaifu vya upinzani zimepita. Sas vyama vinafwatilia mambo kitaalamu. Ngoja tuone itakuaje. Kaka Deo habari haijasema kuwa shitaka lilikua ni nini. Tujuze kwa kina

    ReplyDelete
  2. Pole ndugu yangu Kafumu rudi kwenye taaluma yako kwani siasa ni mchezo mchafu. Wewe ulifanya kampeni yako kistaarabu ila wenye kujua siasa wamekuharibia. Hukumu hii ni tamu kwa kutoa funzo kwa chama tawala kwamba hawako juu ya sheria. Taratibu za uchaguzi ni kwa kila mtu.Hakika mbinu zile za kupandikiza udini, kuhonga vyakula, blackmail ya daraja na kadhalika kwa wananchi wenye shida ni mchezo mchafu sana kufanywa na chama nambari wani.

    ReplyDelete