BM BARBERSHOP KINONDONI

Sunday, August 12, 2012

AGNES MASOGANGE ACHA KUTUMIA JINA LANGU KUTAFUTA UMAARUFU ASEMA SINTAH


Binti wa Kipare ambaye amewahi kuvuma miaka kadhaa iliyopita na kupamba vyombo vingi vya habari hasa Magazeti ya UDAKU Christina Manongi 'Sintah' ambaye siku za karibuni aliripotiwa kusambaza picha za UTUPU za mwanadada anayeibuikia kwenye TASNIA ya uimbaji Agness Gerald Masogange. Sintah ni motto wa kwanza wa Mzee John Manongi anayeishi Sinza mwenyeji wa KIHURIO mkoani Kilimanjaro Wilaya ya Same. Muigizaji huyu aliyetengeneza jina kupitia kikundi cha Kaole Sanaa Group amempiga mkwara mzito Masogange na kumuambia AFUNGE BAKULI LAKE kwani akiendelea atatoa picha zake za UTUPU moja baada ya nyingine ili kumnyamazisha Kabisa.

Sintah ambaye alikulia eneo la KINONDONI SHAMBA kwa shangazi yake ajulikanaye kwa Jina la Mama Shem aliongea na Mwanatanga kwenye Saloon ijulikanayo kama Twins Saloon iliyoko Kinondoni Muslim mbele ya Dada yake aliyejitambulisha kwa jina la Sakina Shem na kuapa kumdhalilisha zaidi binti huyo Masogange kama ataendelea kumfuatafuata. Aidha muigizaji huyu mwenye  mbwembwe nyingi  kutoka ndani ya  tasnia ya filamu za Kibongo amemtaka  video queen wa Bongo Agness Gerald Masogange   kuacha kumsingizia kwenye SAKATA hili la picha za utupu kwakuwa yeye hahusiki.

Sintah amesema kuwa amesikitishwa  sana na kitendo cha  Agness kumtaja yeye (Sintah) kuwa ndiye anahusika na kuisambaza kwenye mitandao video  inayomuonyesha Agness akiwa mtupu huku pia akionekana kufanaya  matendo kadhaa ya kingono.

"Nimemsikia na isitoshe kuna watu wengi wameniambia juu ya hilo la kunitukana na kunitaja redioni kuwa nahusika, mimi  sijui lolote awaulize marafiki zake  ambao mimi naamini ndiyo wanahusika kuzisambaza kwani hata kwenye BBM yangu ni wao ndiyo walinitumia namuomba afunge bakuli  lake la siivyo nitazitoa zaidi kwani ninazo pati wani mpaka 3 na zote nimetumiwa na marafiki zake ambao yeye anacheka nao lakini hajui kama ni ma-sn***ch" alisema Sintah. 

Akiendelea zaidi Sintah amefunguka kuwa  kamwe hajui lolote kuhusu kamera anayoisema Agnes, kwani binafasi hajawahi kukutana naye  na  alimjua  kupitia   nyimbo za wasanii wa Bongo Fleva kwa kuwa msichana huyo anapenda kuuza sura  na zaidi hajui hata  anapokaa.

Aidha mwanatanga alimuuliza Sintah swali la kizushi kuhusu hali yake ya NDOA ambayo ilifanyika miaka kadhaa nyuma kati yake na kijana wa Kiganda na send off Part yake kufanyika pale Msasani Beach Club na kushuhudiwa na mamia ya marafiki zake na baadaye Wedding mjini Kampala Uganda. Sintah alijibu kuwa hayo ni maisha binafsi wala hayahusiani na mada inayozungumziwa. Swali hili la kizushi lilikuja baada ya Tetesi kuwa anamahusiano ya Kimapenzi na Mchezaji wa Simba SC Emmanuel Anthony Okwi. Katika hili alidai kuwa kwani kuna ubaya gani mimi kuwa mahusiano na OKWI??? Kauli hii iliendelea kuacha tungo tata na mwanatanga kuamua kuachana na hili kwakuwa lengo si kuingilia maisha ya mtu kwa undani.

No comments:

Post a Comment