BM BARBERSHOP KINONDONI

Sunday, August 12, 2012

MASHUJAA MUSICA WAENDELEZA KUAMINI KUWA BENDI YAO ITAPATA JINA KUPITIA TWANGA PEPETA PEPETA

Bendi ya Mashujaa Musica imemtambulisha mcheza shoo Super K ambaye alikuwa Umangani akicheza shoo baada ya kuwa nje ya ULINGO wa Twanga Pepeta kwa miaezi Sita akiwa huko Uarabuni akicheza Shoo kwenye kumbi za Hoteli. Ushawishi wa Super K kuhamia Mashujaa ulifanywa na Rais wa Bend hiyo Charles Gabriel Mbwana (Torres) ambaye alikutana na Super K Dubai alipokwenda miezi zaidi ya minne iliyopita wakati akiwa safarini kuhamia Mashujaa Band.

Uongozi wa ASET ulilitambua hili tangu wakati huo na Super K aliongea na mwanatanga kuhusu kuhamia kwake Mashujaa kwa Dau ambalo ni pesa aliyokabidhiwa siku alipotua Airport akitokea Uarabuni wiki kadhaa zilizopita. Aidha Super K alifika kwenye Mazoezi ya bendi ya Twanga Pepeta siku ya Jumanne na kukuta mazoezi yakiendelea huku kukiwa na Wacheza shoo LUKUKI ambao watatambulishwa PUNDE baada ya Ramadhani. Super K aliambiwa na Asha Baraka kuwa RUKSA kwenda unakotaka ili ukatafute maisha sisi tupo na tunaendelea KUJIKONGOJA. Kauli hii ilimfanya Super K atabasabu na kukana kutojiunga na Mashujaa lakini kila Mwanamuziki aliyekuwepo siku hiyo ya mazoezi alibariki safari ya mcheza Shoo huyu na kusema kuwa Twanga Sera zake sasa nikuwa na Safu ya Wacheza Shoo wa Kike na ndiyo maana haijaongeza Mcheza shoo wa kiume hata mmoja tangu kuondoka kwa kina Nyamwela, Danger Boy na sasa yeye Supr K.

"Uwanja uko wazi kwa yoyote anayeona anataka kwenda kutafuta maslahi kwakuwa Twanga haina Fedha chafu" alisema Mama Asha Baraka. Wiki hii imeripotiwa kuwa Mcheza Shoo Lilian Internet na Mpiga Gitaa Ally Akida waliokuwa Twanga Pepeta na kuhamia Mashujaa wameachana na Bendi hiyo na kuamua kurejea Twanga Pepeta. Uongozi wa Mashujaa na Twanga pepeta uliulizwa na yafuatayo ni Mahojiano juu ya Jambo hilo.

Mwanatanga ilijaribu kumtafuta Ally Akida na kumuuliza kama ifutavyo – Mzee wa Bunju vipi mbona nasikia huonekani kazini takribani Mwezi sasa kwenye Bendi yako ya Mashujaa???
Majibu ya Ally Akida- Kaka nimeamua kuachana na bendi ya Mashujaa Musica kwasababu hawana roho ya huruma mimi nilikuwa namuuguza mwanangu viongozi wote walikuwa na taarifa nashangaa wamenikata kiasi cha shilingi elfu sitini (60,000) kwenye mshahara wangu si utapeli huu bora nikae nyumbani nifanye mambo yangu binafsi.

Swali kwa Mashujaa Musica- Uvumi wa Ally Akida kuikacha Bendi yako kwa madai ya kukatwa pesa yake ya mshahara una ukweli ndani yake??? 

Mashujaa Musica - Kuhusu Ally Akida ni kweli hayuko kazini mwezi sasa,hata ivyo suala lake bado liko ofisini na hajaacha kazi rasmi kwani ana vitu vya kukabidhi kama ni kweli, Na kuhusu Liliani ni uvumi huo labda unatokana na yeye kuomba likizo ya Ramadhani huo ni uzushi. Ndiyo maana nina uhakika ni uzushi na kuhusu Ally Akida hajatoa taarifa rasmi hivyo bado ni mfanyakazi mpaka hapo atakapoandika rasmi barua ya kuacha kwani ana mkataba, hata hivyo tuko tayari kumuachia kama akitamka rasmi na si kupitia katika magazeti;DEO unajua strategically ilikuwa lazima kuboost jina through big names lakini trust me mipango ya baadae ya bendi ni jina la bendi kwanza na through the reputed name we can nurture the young talented...

Swali kwa ASET- Ni kweli Ally Akida anataka kurejea Twanga Pepeta, na vipi kuhusu Lilian Internet kuwepo kwenye Mazoezi ya Twanga Pepeta??? 

Jibu kutoka ASET- Kaka Deo Twanga ni Bendi kubwa watu wanatoka na wengine wanaingia na wale wanaotoka baadaye hurejea hivyo hilo si jambo geni kwenye Bendi hii Kongwe. 

Majibu haya yalinipa Picha ya kutaka kujua kitakachofuata… Twanga wameahidi kuendelea kufanya kazi na kutaka niwe na subira hadi mwezi MTUKUFU uishe.

No comments:

Post a Comment