BM BARBERSHOP KINONDONI

Sunday, August 12, 2012

HILI NDILO TAMKO LA YANGA KWA RAGE


Uongozi wa klabu ya yanga umeshangazwa na kauli ya mwenyekiti wa Simba Alhaji Ismail Aden Rage baada ya klabu ya Simba kushindwa kumsajili mlinzi wa APR ya Rwanda Mbuyu Twite.

Katibu wa Yanga John Selestine Mwesigwa amesema Mwenyekiti wa Simba Rage ameshindwa kufanya usajili kwa kwenda na mfumo wa sasa wakati huu badala yake akitaka kusajili kwa mlango wa nyuma. Kwa mujibu wa maelezo ya Mwesigwa amesema Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kumfuatilia Mbuyi Twite hata kabla ya kuanza kumfuatilia Kelvin Yondani na Simba ndio waliokuwa katika mbio za kuizunguka Yanga Jambo ambalo hata hivyo Simba imegonga mwamba.

Mwesigwa amemtaka Mwenyekiti wa Simba awaambie ukweli wanachama na wapenzi wa klabu yake kilichotokea na vipi wameshindwa kumsajili mlinzi huyo raia wa DRC badala ya kutupa lawama kwa uongozi wa Yanga na TFF. Mwesigwa amesema ingekuwa Simba imemsajili kweli Mbuyu Twite basi mfumo wa kuhamisha wachezaji wa Computer (transfer management system (TMS) ) ungeonyesha na kukataa data za Yanga kumsajili lakini Simba wakionekana kutokuwa na taarifa kupitia mfumo huo jambo ambalo mwenyekiti wa Simba halifahamu na ameshindwa kulielezea hilo.

Katika hatua nyingine Mwesigwa amesema Yanga haiko tayari kushughulikia madai ya Simba kurejeshwa pesa walizompa mlinzi huyo kwani wao kama Yanga hawafahamu lolote juu ya hilo.

No comments:

Post a Comment