BM BARBERSHOP KINONDONI

Sunday, August 12, 2012

UFAFANUZI WA PANGO LA MAFISANGO HUU HAPA

UFAFANUZI WA PANGO LA MAFISANGO HUU HAPA
Klabu ya Simba ambayo ndiyo mwajiri wa aliyekuwa kiungo wa klabu hiyo marehemu Patrick Mutesa Mafisango Papaa imetoa ufafanuzi juu ya kutolewa nje kwa vyombo vya marehemu Mafisango katika nyumba iliyoko maeneo ya Chang’ombe jijini Dar es salaam.

Afisa habari wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amekiri kuwa ni kweli vyombo vya marehemu Mafisango vilitolewa nje ya nyumba aliyokuwa anaishi marehemu lakini hilo halihusiani moja kwa moja na Simba kwasasa kwani wakati vyombo hivyo vinatolewa nje tayari mkataba wa Simba na mwenye nyumba hiyo ulikuwa umemalizika tangu mwezi wa june 2012.

Kamwaga amesema tangu mkataba huo unamalizika pango hilo lilikuwa chini ya mdogo wake marehemu ambaye amekuwa akiishi na Mafisango tangu marehemu akiwa katika klabu ya APR ya Rwanda na baadaye Azam FC kabla ya kuichezea klabu ya Simba. Mdogo wa marehemu aliomba kuendelea kusalia hapo na kuendelea kutumia vyombo vya marehemu Mafisango na Simba kwa kutambua udugu na ukaribu wa wanandugu hao iliamua kumuachia vyombo hivyo lakini kwa makubaliano ya kutokuendelea kulipa pango hilo mara baada ya mkataba wa nyumba hiyo kumalizika mwezi wa sita.

Tangu wakati huo mdogo wake na marehemu aliendelea kuishi katika nyumba hiyo na huku akiwakaribisha ndugu jamaa na marafiki karibu saba ambao wote ni wa Congo DRC.Taarifa zinasema kuwa kulikuwa na makubaliano mengine kati ya mwenye nyumba na wakongo hao ambao mpaka wanatupiwa virago hakukuwa na malipo yoyote yaliyofanyika jambo ambalo limemfanya mwenye nyumba huyo kushindwa kuendelea kutoa hisani.
 

No comments:

Post a Comment