BM BARBERSHOP KINONDONI

Monday, August 6, 2012

KALALA JUNIOR AFUNGUKA

BAADA YA UKIMYA WA MUDA MREFU HATIMAYE KALALA JUNIOR AAMUA KUFUNGUKA HIZI NI JUHUDI BINAFSI KATI MWANATANGA NA DADA YAKE KALALA JUNIOR BI. MARIA EMMANUEL KALALA.
 
NAMNUKUU KALALA " Kaka Deo Mutta nakuheshimu sana mimi nimeamua kupumzika Muziki kidogo ili nijipange kwa ajili ya Shule na Biashara, Ninasikia tetesi nyingi sana mara Ninaenda Twanga Pepeta,  Mara ninaenda  Mashujaa Musica  mara  Extra Bongo yote nayasikia.  Mimi nimeamua kupumzika na kusimamia Jengo langu kule BOKO ambalo sasa linaelekea Ukingoni. Pili nimeamua kufanya biashara kufuatia Mafao yangu baada ya Mgao kutoka Band ya Mapacha Watatu ambako nilikuwa ni Hisa pale kama Mkurugenzi. wiki hii nasafiri naenda China na Dubai kwa ajili ya Maandalizi ya Kibiashara. Unayoyasikia mtaani hayana ukweli wowote na wala sina mpango wa kufanya Muziki kwasasa zaidi ya kutoa Albam yangu Binafsi itakayowashirikisha baadhi ya Wasanii Nguli wa Muziki wa Kizazi Kipya na Dansi. Muziki ninaupenda ninaweza nikarejea kama mambo yangu ya kibiashara yatakapokuwa yametengemaa. Anayetaka kujua habari zaidi anitafute Mwenyewe Kalala Junior na sikueneza habari zisizo na Ukweli wowote. Kinywa changu ndiyo Msemaji wangu. Natarajia kupata Mshauri wa kimaisha na Punde nitamtangaza Hadharani na huyu atanisimamia kwenye kila Jambo.. iwe kimziki au kibiashara.; Naomba Washabiki wangu wajue hivi nawewe kaka yangu tambua hivi pia. Wakati ukifika nitawajulisha wadau na Mashabiki wangu kwenye Media Zote kuhusu HATIMA yangu Kimziki. Mbona rafiki yangu wa Karibu MRISHO NGASSA kaamua kwenda Simba BADALA YA YANGA??? hata miye si ajabu kuwa Mfanyabiashara. Nikirejea kwenye Muziki kila mtu atajua na nitakuja kivingine kabisa." MWISHO WA KUNUKUU.

No comments:

Post a Comment