BM BARBERSHOP KINONDONI

Monday, August 6, 2012

MANENO SABA YA MANJI WAKATI WA KUAPISHWA

MWENYEKITI MPYA WA YANGA AKILA KIAPO MBELE YA MZEE KATUNDU
 Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam Mheshimiwa Yusuph Mehboob Manji aliapishwa rasmi juzi Jumapili katika Ukumbi wa Diamond Jubilee na Mzee Katundu yeye na Viongozi wenzake akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Yanga Ndugu. Clement Sanga pamoja na na Wajumbe wengine ambao wanaunda Jopo la Kamati ya Utendaji mbele ya Mke wa Marehemu Raisi wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume. Wakati anaapishwa alitoa tamko ambalo leo limewasilishwa rasmi kwa Vyombo vya habari na kutamka bayana masuala saba muhimu ya kuzingatiwa kama Ifuatavyo:

1.   Uongozi wa Klabu ya Yanga utakuwa unaongea na Waandishi wa Habari mara moja kwa mwezi.

2.   Masuala yote ya kiufundi yatakuwa yakizungumzwa na Kocha kabla na baada ya mechi hivyo Uongozi    hautahusika na taarifa zozote kwenye eneo hilo kwakuwa viongozi waliopo hawakuja Yanga kutafuta Umaarufu bali kujenga Klabu. 

3.  Masuala yote ya Klabu naya Kiutawala yatazungumzwa na Afisa Habari wa Klabu kwakuwa ndiyo kazi yake.

4.  Klabu ya Yanga imefuta Posho zote za Vikao kuanzia leo 05/08/2012 ili kupunguza mzigo kwa Klabu na tunatafuta vyazo kwaajili ya kupata swastani wa shilingi milioni 570 kwa mwezi kwa ajili ya kuendeshea club yetu.

5.  Kamati zote zilizokuwepo kwenye uongozi ulipopita zimevunjwa rasmi na utaratibu wa kuunda zingine ambazo zitakuwa na TIJA kwa Klabu zitaundwa Punde.
 
6.  Suala la Ujenzi wa Uwanja wa Yanga litaundiwa Kamati Maalum ya kuratibu zoezi hilo.

7.  Uongozi wa Yanga utahakikisha kuwa kila aliyeajiliwa na Klabu ya Yanga kuanzia Kocha Mkuu, Makocha Wasaidizi, Katibu, Afisa Habari  na Wachezaji wote wanalipwa mishahara yao (STAHIKI) kwa wakati.
 
Ahsanteni sana YANGA KWANZA MTU BAADAYE !!!!!!!!!!!!!!!!!
MWENYEKITI MPYA WA YANGA YUSUPH MANJI AKIPONGEZWA NA MAMA FATMA KARUME BAADA YA KULA KIAPO

No comments:

Post a Comment