BM BARBERSHOP KINONDONI

Friday, August 24, 2012

MSAMA PROMOTIONS TFF, SIMBA KUWENI NA HAYA ALPHONCE MAODEST AMETOA MCHANGO MKUBWA SANA KWENU CHANGIENI MATIBABU YAKE

Alphonce Modest, anavyoonekana kwa sasa.
Nimesoma habari kupitia gazeti la Championi kuhusu hali mbaya ya kiafya ya mchezaji mkongwe aliyewahi kuchezea Simba kwa mafanikio makubwa na pia kucheza Taifa Stars kwa kipindi kirefu sana tena kwa kiwango cha juu Alphonce Modest.

Mchezaji huyu kwa mujibu wa Gazeti la Championi anasumbuliwa na figo na alikuwa amelazwa Bugando Mwanza na hali yake kimaisha ni mbaya kumudu matibabu. Alphonce Modest amewataja Juma Kaseja na Mrisho Ngassa kama wachezaji pekee wanaomsaidia. Namkumbuka mchezaji huyu alivyokuwa na nidhamu kubwa,mpole na mtu wa dini na hasa soka lake akiwa moja ya beki namba tatu bora kuwahi kutokea Tanzania.
Hali ya soka huko nyuma kifedha ilikuwa mbaya zaidi ya sasa na wachezaji wengi wamebaki maskini.
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama (kushoto) akimkabidhi msaada wa fedha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni moja mchezaji wa zamani wa Simba, Mtibwa na Taifa Stars, Alphonce Modest kwa ajili ya kumsaidia katika matibabu ya ugonjwa wa mifupa unaosababisha miguu kufa ganzi ‘yabisi baridi’.

Naomba nitoe wito kwa TFF ifanye juhudi za kumsaidia Alphonce Modest ikibidi uwekwe utaratibu wananchi tumsaidie kuchangia tulicho nacho ili Modest ajue tunathamini mchango wake ktk Taifa hili na iwe motisha kwa vijana tunaowahimiza washiriki michezo.

Pole sana Alphonce Modest,Mungu mwenye huruma akupe nafuu ya haraka ili uendelee kujenga Taifa letu. Kampouni ya Msama Promotion imekuwa ya Kwanza kuchangia Matibabu ya Mchezaji huyu kwa kutoa Jumla ya shilingi milioni moja kupitia Mratibu wa Tamasha la Injili la Pasaka Tanzania, Alex Msama Mwitta. TFF pamoja na Simba Sports Club oneni aibu na tambueni mchango wa Modest kwa kumsaidia kupata matibabu. Said Kilumanga Mtanngazaji wa Channel Ten pamoja na Saleh Ali ndiyo wahamasishajiwakubwa wa zoezi hili la uchangishaji wa matibabu ya Modest. Mungu mpe afya na apone kwa haraka. Alex Msama akielezea jinsi alivyoguswa hadi akaamua kumsaidia Modest na kutoa mwito kwa Watanzania kumuunga mkono kwa kumsaidia mchezaji huyo wa zamani ambaye anahitaji fedha za kumtibia katika taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)
 
Modest anasumbuliwa na ugonjwa huo tangu mwaka 2011. Kwa yeyote aliyeguswa na tatizo lake awasiliane na Mtangazaji wa Channel Ten, Said Kilumanga (wa pili kulia) kwa kupitia simu namba 0718 427426 au Mhariri Kiongozi wa Champion, Saleh Ally. 


Alphonce Modest akitoa shukrani kwa Msama na kuelezea jinsi ugonjwa huo ulivyompata na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza kwa mwaka mzima wa 2011.
Said Kilumanga ambaye ni mmoja wa wahamasishaji, waliowezesha kupatikana msaada huo kutoka kwa Msama, akiendelea kuhamasisha umma kumsaidia kwa hali na mali Modest apate kupona.
Saleh Ali ambaye pia ni mmoja wa wahamasishaji, akiwaomba wasamaria wema kuendelea kumsaidia Modesti kwa hali na mali
Alphonce Modest akitembea kwa taabu huku akisaidiwa na mdogo wake Francis.


1 comment:

  1. Tumchangieni Alphonce Modest jamani huu ndio ubinadamu.Tulimshangilia enzi zake akiwa na timu ya taifa sasa anaumwa sio kumwachia Kaseja na Ngassa kwa uzuri wa roho zao jukumu lote. TFF wacordinate na wao kutoa msaada. Halafu TFF waweke sera ya kuwasaidia wote waliowahi kuchezea Taifa. Sio mchezaji anakua hoi bin taaban halafa wao wanakula ganzi.

    ReplyDelete