Wakati akifunga kikao cha Bunge cha jioni ya
leo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anne Makinda
aliwatangazia Wabunge kuwa Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Abdallah Juma Abdallah Saddallah
amepata ajali katika eneo la Tumbi, Kibaha Mkoani Pwani akiwa njiani kurejea
Dar es Salaam, ndani ya gari hilo alikuwemo Dereva wake, Naibu Waziri, Watoto
pamoja na Msaidizi wa shughulil za nyumbani. Spika alitoa taarifa kuwa majeruhi
waliwahishwa hospitali ya Tumbi, Kibaha kwa matibabu zaidi.

Imeelezwa kuwa baada ya ajali hiyo umati wa wananchi wakiwemo vibaka walifika eneo hilo kutaka kupora mali mbali mbali ila hawakuweza kufanikiwa baada ya raia wema kusaidia kuepusha hali hiyo .Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo baada ya kuhojia na mwandishi wa habari hizi na kuwa hali ya naibu waziri huyo si mbaya sana zaidi ya dereva wake ambaye ameumia kichwani.".
No comments:
Post a Comment