BM BARBERSHOP KINONDONI

Thursday, August 9, 2012

NYASA TIMES WATANGAZA VITA NA TANZANIA


RAISI JOYCE BANDA WA MALAWI
Na. Cedrick Ngalande wa Nyasa Times
Muda mchache baada ya kupata Uhuru watu wachache kutoka Tanzania walitaka kudai eneo kubwa la Ziwa Malawi au Ziwa Nyasa kuwa liko upande wa Tanzania. Vichwa makini wakati huo vya Watanzania akiwemo Rais Julius Nyerere, walielewa umuhimu wa kuheshimu mipaka iliyowekwa wakati wa utawala wa Kikoloni.
HUYU NI CEDRICK NGALANDE WA NYASA TIMES MUANDISHI WA MAKALA HII KWA KIINGEREZA NA KUTAFSIRIWA KWA KISWAHILI ILI KUSAIDIA WATANZANIA WENGI KUELEWA ALICHOKUSUDIA MUANDISHI HUYU
Wakati wa utawala wa Hayati Dr Kamuzu Banda, Tanzania haijawahi kuendeleza mdahalo huu wa kijinga wa kutaka kuliteka Ziwa Malawi/Nyasa. Suala hili pia halikuweza kufanyiwa kazi wakati wa Utawala wa Raisi Dr Bakili Muluzi na wote waliofuata baada yake. Wakati wa utawala wa Dr Bingu wa Mutharika aliamua kuipatia Kampuni moja kufanya utafiti wa Mafuta kwenye Ziwa hilo. Tanzania haikusema chochote wakati utafiti huu ulipoanza kufanyika. Wakati huu tukiwa na rais Mpya Mwanamke ghafla Serikali ya Tanzania wanaitaka Serikali yetu isimamishe shughuli zote za kitafiti kwenye Ziwa Malawi/Nyasa mpaka suala la mipaka litakapojadiliwa na kuwekwa vizuri. Kwanini Sasa????
 Wananchi, kuna sababu kwanini Wamalawi tuna Utamaduni. Utamaduni utakuwa hauna maana au unaweza kuwa umepitwa na wakati lakini ni muhimu kwakuwa ulianzishwa muda mrefu uliopita hivyo uheshimiwe. Kwenye Siasa kuna kitu kinaitwa ITIFAKI YA RAIS (‘presidential protocol’). Kuna vitu vidogovidogo ambavyo kwa miaka mingi vimeonyesha kuwa nivizuri na Raisi anaweza au asiweze kuvifanya ili kuwakilisha nchi yake vizuri na kwa usahihi kuepuka mizozo isiyo ya lazima.

MTIHANI WA RAIS JOYCE BANDA KUKABILI UTATA HUU WA MPAKA KIDIPLOMASIA
Unaweza kudhani kuwa wengine mengine si muhimu lakini ni muhimu sana. Baadhi ya masuala hayo ni kama ifuatavyo;
  1. Rais hawezi kuwasema  maraisi wenzake vibaya hadharani,  
  2. Raisi hawezi kumsindikiza Rais mwenzake kwenda kwenye gari;
  3. Marais hutembea na majeshi kama ngao kwa ajili ya kulinda miradi yao ya Kinchi.
  4. Maraisi huwa na rangi moja isiyoyumba na kubadilika kwakuwa inaonyesha kujiamini.
  5. Kama Maraisi wawili wakiwa wanasalimiana huangaliana usoni na kila mmoja atahakikisha anaangalia Kamera ili kupata picha inayowakilisha kujiamini mbele ya mwenzake.
  6. Rais akiwa anamsindikiza Rais mwenzake atahakikisha anakuwa wamwisho kuingia mlangoni, hii ni ishara ya Kiulinzi na kiusalama.
  7. Kuna Clip moja ya Video inayomuonyesha Mwenyekiti  Yassier Arafat na Waziri Mkuu Ehud Barak. Clip hii inamuonyesha Ehud Barak akiwa wa mwisho kuingia kwenye chumba pale  Camp David.
  8. Clip nyingine inayoonyesha Raisi George W Bush wa Marekani akimsukuma Waziri Gordon Brown kutangulia pale Number 10 Downing Street. Tendo hili liliwachukiza sana baadhi ya wanasiasa wa Uingereza (British political experts).
 Ikumbukwe kuwa hadhi ya Kiraisi ni MCHEZO (Game) kwakuwa sura iko mahali popote kidunia kwenye siasa.  Sura ya Nchi inatafsiriwa zaidi kwa muonekano wa Mtawala (Raisi) kwenye utawala wake. Raisi Barak Obama huwa anapenda sana kuwashika Maraisi wenzake begani wakati wakusalimiana. Unaweza ukadhani kwamba huwa analifanya kwa bahati mbaya na hakuwa amelipanga. Hebu jaribu kukumbuka jinsi baba yako alivyokuwa akikushika bega ulipokuwa mtoto mzuri. 

Inasemekana kuwa Raisi Bill Clinton alishindwa kupata muitikio mzuri kwenye summit na Boris Yelsin wakiwa Moscow kwasababu Raisi Clinton aliteguka Enka wakati anaingia Moscow. Hivyo ilibidi aingie na wheelchair kwenye summit. Muonekano wa kigonjwa wa Raisi huyu wa Marekani wakati huo ulipunguza umuhimu kwa wake kwa Boris Yelsin. 

Inasemekana kuwa Ghana ilirejesha heshima yake huko Afrika ya Magharibi  wakati Raisi Jerry J. Rawlings alipowasili kwenye Mkutano wa 25 wa OAU nchini Togo Mwezi Julai 2000 akiwa kwenye Vazi la KIJESHI lililoonyesha Kujiamini kwa Raisi huyu KIJESHI.

MUONEKANO WA RAISI NJE YA NCHI YAKE.  RAISI ANAJIONYESHAJE??? RAISI ANAZUNGUMZAJE?? JE NI MUHIMU SANA????
Wakati Joyce Banda akichukua Madaraka ya Uraisi ilionyesha wazi kama vile Malawi sasa itakuwa ikitekeleza yote yatakayoelekezwa na Nchi jirani kwa dhana ya kuwa yeye ni Mwanamke. Kuna baadhi ya magazeti ya Kiingereza walishangazwa sana na kutuita ‘a donor fearing nation’.Raisi Joyce Banda alipoenda Landani Uingereza alimuinamia Malkia Elizabeth wakati anamsalimia. Kitendo hiki kiliwashangaza sana watu na Dunia Nzima kuwa kwanini alifanya hivyo wakati wote ni viongozi wa Nchi??? Haya yote yameonyesha kuwa sura ya Utawala wa Malawi niwakioga ulio na uwanajike ndani yake. Dunia ilianza Kusikia Mnuko wa Damu kutokea Malawi baada ya Mwanamke kuingia madarakani. Sasa Tanzania imeamua na kuona kuwa huu ndiyo wakati muafaka wa kuligawa Ziwa Malawi/Nyasi. Kumbuka kuwa wazo hili halijawahi kuletwa wakati wa utawala wa Muluzi au  Mutharika wakiwa Madarakani.
ZIWA MALAWI/NYASA
 Kama tukiruhusu wazo hili la Tanzania kudai ubainishaji wa Mipaka sasa, kitakachofuata ni kudai pia na Chitipa?  Msumbiji watadai Mlima wa Mulanje?
Serikali ya Malawi lazima iweke wazi kuwa hakuna sehemu au eneo lolote nchini Malawi ambalo litafanyiwa Majadiliano - full stop! Ni wakati wa Serikali ya Malawi kuonyesha kujiamini. Waambie Tanzania kwamba Ziwa Malawi lilikuwa, ni na litaendelea kuwa la Wamalawi.
Cha kushangaza ni kwamba mbali na kauli mbalimbali za Tanzania Serikali yetu haionyeshi reaction ya aina yoyote badala yake. Waziri wetu wa Mambo ya Nje wa Malawi ametoa kauli kuwa suala hili litajadiliwa, Wewe Waziri?? Kwanini Hivyo?? Je unapanga kuwapatia Watanzania eneo ambalo si mali yao??? Je Unampango wa kuligawa Ziwa?? Kwanini unaleta maamuzi ya kirafiki yasiyo na maslahi kwa Wamalawi??? HAIWEZEKANI NA HATUTAKUBALI.

2 comments:

  1. Huyo mwandishi ana agenda ya uchaguzi wa rais Malawi. Anajua kwamba Lazima Malawi iridhie ukweli kwamba Tanzania inamiliki sehemu ya mashariki ya ziwa Nyasa. Huyu mwandishi ni adui ya usawa wa kijinsia kwa kuandaa ajenda kuonyesha rais wao ni dhaifu kwa kuwa ni mwanamke. Mtu mbaya sana.

    ReplyDelete
  2. Picha ya chini: Eti hao jamaa walioko beach wakitumbukiza mguu tu ndani ya maji wako Malawi. Hata hapo walipoketi wakati wa high tide ni Malawi,laah mpaka gani..

    ReplyDelete