Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipitisha Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu mwaka
1992. Tangu wakati huo, maendeleo mapya yamekuwa yakitokea kitaifa na kimataifa
ambayo yana athari ya moja kwa moja kwenye masuala ya Idadi ya Watu na
Maendeleo. Hii imefanya serikali ipitie upya Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu ili
kujumuisha maendeleo hayo mapya.
Ndani ya
nchi, uchumi umebadilika sana kutoka ule uliokuwa ukipangwa na serikali kuu
kuwa uchumi wa soko unaozidi kutawaliwa na sekta binafsi, ambayo ina dhima
kubwa katika masuala ya idadi ya watu na maendeleo. Zaidi ya hayo, mnamo Juni
1999, serikali ilizindua dira mpya ya maendeleo, yaani, Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2025. Sera hii iliyodurusiwa, yaani Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu ya
mwaka 2006 ina lengo la kuratibu na kuhusisha sera, mikakati na programu
nyingine ili kuhakikisha maendeleo endelevu ya watu na kukuza usawa wa kijinsia
na uwezeshaji wa wanawake. Itatekelezwa kwa mkabala jumuishi wa sekta
mbalimbali kwa upana zaidi. Aidha,
Serikali
itashirikiana na Asasi Zisizo za Serikali (AZISE), sekta binafsi, jumuiya na
mawakala wengine wanaotekeleza sera. Kwa hakika, watu binafsi, vyama vya siasa
na makundi mengine katika vyama vya kiraia vinatarajiwa kuwa na dhima ya kuhakikisha
kufikiwa kwa malengo na madhumuni ya sera. Madhumuni makuu ya dira ya maendeleo
ya nchi ni kuwaondoa Watanzania kutoka kwenye umaskini na kuinua ubora wa
maisha ya watu. Kwa hiyo, Sera inatoa miongozo ya kushughulikia masuala ya
idadi ya watu kwa namna jumuishi.
Hivyo,
inatambua mahusiano baina ya mienendo ya idadi ya watu na ubora wa maisha kwa
upande mmoja na ulinzi wa mazingira na maendeleo endelevu kwa upande mwingine.
Utekelezaji wake utatoa upeo mpya kwa programu za maendeleo kwa kuhakikisha
kwamba masuala ya idadi ya watu yanashughulikiwa kikamilifu. Ni matumaini yangu
kwamba, kwa kuungwa mkono na kwa ushiriki kamilifu wa watu, utekelezaji wa sera hii utafanikiwa.
Historia ya Sensa Tanzania.
Sensa ya
kwanza Tanzania ilifanyika mwaka 1910. Sensa nne za Mwisho zilifanyika baada ya
Uhuru, katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na 2002. Kulingana na sensa ya mwisho
iliyofanyika mwezi Agosti 2002, idadi ya watu nchini Tanzania ilikuwa
34,443,603.
MATOKEO YA SENSA YA WATU 1967-2002 NA MAKADIRIO KATI YA MWAKA
2003-2025 1967-2002 NA MAKADIRIO KATI YA MWAKA
MWAKA IDADI
1967 12,313,469
1978 17,512,610
1988 23,095,885
2002 34,443,603
IDADI YA
KUANZIA MWAKA 2003-2025 MAKISIO
2003 34,859,582
2004 35,944,015
2005 37,083,346
2006 38,250,927
2009 41,915,880
2010 43,187,823
2012 45,798,475
2015 49,861,768
2020 57,102,896
2025 65,337,918
Maswali yaulizwayo mara kwa mara (Frequently Asked Questions)
Sensa
ya Watu na Makazi ni nini?
Jibu
la Swali hili-Sensa ya Watu na Makazi ni utaratibu
wa kupata na kurekodi habari kuhusu watu na makazi yao.
No comments:
Post a Comment