BM BARBERSHOP KINONDONI

Monday, September 10, 2012

AUNT LULU ACHEZEA VITASA MANGO GARDEN



Na Richard Bukos

NI aibu! Mtangazaji ambaye pia ni mwigizaji wa filamu za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ anadaiwa kubondwa wakati akigombea penzi la pedeshee maarufu jijini Dar. Kwa mujibu wa shuhuda wetu, Aunty Lulu alichezea kichapo hicho kutoka kwa mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Fatma, usiku wa Alhamisi iliyopita kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar ambapo Kundi la Mashauzi Classic lilikuwa likifanya makamuzi.

Shuhuda huyo makini aliyeshuhudia mtiti mwanzo hadi mwisho alidai kuwa wawili hao kwa muda mrefu walianza kurushana roho ukumbini hapo huku kila mmoja akimpiga kijembe mwenzake.
Alidai kuwa baada ya vita baridi ya maneno, wawili hao walipandwa na hasira ndipo wakavaana na kuanza kupeana kichapo huku Aunty Lulu akizidiwa na makonde hadi walipoamuliwa lakini msanii huyo akawa ameshakula makonde ya kufa mtu.

Ijumaa Wikienda lilipofika eneo la tukio lilizungumza na wawili hao kuhusiana na kumgombea pedeshee huyo (jina linahifadhiwa) ambapo kila mmoja alijitapa kuwa mwenzake hana jeuri ya kushea naye mapenzi.Chanzo:www.globalpublishers.info

1 comment:

  1. Uonevu wa kijinsia: Kwa nini Pedeshee (PDG= President Directeur General)huyo hajatolewa picha na jina lake? Ingefaa kuwaanika wote sio kumwonea ant lulu kwa kuwa mwanamke. Tunangojea mwandishi amwanike huyo PDG na kama yeye ni CEO wa kampuni gani au ni kina ndama mtoto wa ng,ombe.

    ReplyDelete