BM BARBERSHOP KINONDONI

Sunday, September 2, 2012

BAADHI YA WANAMUZIKI WA BAND YA MASHUJAA WAPATA AJALI KARIBU NA UBALOZI WA MAREKANI

MMOJA WA WASANII WA MASHUJAA ALIYEUMIA SEHEMU ZA USONI KAMA UNAVYOONA
Alfajiri ya leo katika milango ya saa 11 alafajiri baadhi ya wanamuziki wa Bendi ya Mashujaa,Wamepata ajali mbaya ya gari katika eneo la Drive Inn jirani na Ofisi ya Ubalozi wa Marekani...Kwa Mujibu wa habari kutoka kwa mtoa taarifa bwana King Dodoo amesema baadhi ya wasanii wamepata majeraha kadhaa isipokuwa mcheza show mmoja wa kike ndiye kaumia vibaya sehemu za kichwani...aliongeza kuwa majeruhi wote wamefikishwa katika hospitali ya Mwananyamala.kwa ajili ya matibabu na wengine kupata huduma ya kwanza. King Dodoo aliongeza kuwa Wasanii hao walikuwa katika basi aina ya TOYOTA COSTER wakitokea Mbezi Beach ambako walikuwa na onyesho huko. Wakati wanarejea walipita Kawe na kumshusha mmoja wa wasanii wa bendi hiyo na walipofika eneo la Msasani Drive Inn gari lao lilihama njia na kugonga ukuta na hatimaye kusababisha baadhi ya wasaniii wa bendi hiyo kuumia vibaya..Dereva wa gari hiyo hajulikani alipo....

Poleni sana na Mungu awape Wepesi ili mpone haraka.

1 comment:

  1. Poleni ndugu zetu, mola awasaidie mpone na mrembo pichani apone bila hata sumni ya kovu. Ila mkiwa jukwaani chungeni dereva wenu asistarehe kwa kilevi ama siku nyingine itakua balaa zaidi.

    ReplyDelete