na Sitta Tumma, Mwanza
NDEGE ya
Shirika la Precision, juzi ilikwama kwa muda kutua katika uwanja wa ndege wa
mjini hapa, baada ya fisi kusimama katikati ya njia ya kurukia na kutua ndege.
Tukio hilo la
aina yake limetokea Jumatano wiki hii majira ya saa 2:10 usiku, likihusisha
ndege ya kampuni hiyo iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam.
Mashuhuda wa
tukio hilo walilieleza Tanzania Daima kuwa waliona ndege hiyo ikilazimika
kuruka tena juu ghafla ili kumkwepa fisi huyo ambaye hakujulikana alikotokea,
jambo ambalo lilileta tafrani kwa abiria.
“Wakati ndege
ikianza kutua tulikuwa tunaiona kwa macho yetu. Ghafla tuliiona tena imepaa juu
kuelekea ziwani na baadaye ikapita juu ya uwanja ikielekea mashariki,” alisema
mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.
Alipotakiwa
kuzungumzia tukio hilo, meneja wa uwanja wa ndege wa Mwanza aliyetajwa kwa jina
moja la Madale, alikiri kuwepo kwa fisi wengi eneo hilo la uwanja na kwamba
waliwahi kuuliwa kwa wingi na wanajeshi.
Chanzo: Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment