BM BARBERSHOP KINONDONI

Wednesday, October 31, 2012

BREAKING NEWS!!!!!!!!!!! MBUNGE WA ILALA AKAMATWA KWA RUSHWA DODOMA

BREAKING NEWS FROM TBC TAIFA USIKU WA HABARI!!!!!!!!!!
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu akamatwa kwa tuhuma za rushwa
31/10/2012
Habari kutoka TBC1 zinahabarisha kuwa Mbunge wa Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mussa Hassan Zungu na watu wengine watatu wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa katika Uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM unaofanyika huko Dodoma. Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma. Habari zaidi zinadai kuwa Zungu aliwekewa mtego na TAKUKURU na kubainika akigawa fedha alizokuwa nazo kwenye gari lake na ingawaje gari hilo lilikimbia, mawasiliano ya simu yaliyochukuliwa ni uthibitisho wa tuhuma hizo.
Source: http://www.wavuti.com/4/post/2012/10/mbunge-wa-ilala-azzan-zungu-akamatwa-kwa-tuhuma-za-rushwa.html#ixzz2AuUdEMqm

No comments:

Post a Comment