BM BARBERSHOP KINONDONI

Monday, October 1, 2012

MOTO WATEKETEZA NYUMBA YA YATIMA MOROGORO


Sarah Mgaji, Morogoro Yetu
Nyumba ya watoto yatima iliyopo mtaa wa boma maeneo ya Mazimbu mkoani Morogoro imetekea kwa moto unaodaiwa kusababishwa na shoti ya umeme. Hata hivyo hakuna mtu aliyepoteza maisha ingawa mali za mpangaji na watoto hao yatima vilitekekezwa na moto huo.

Moto huo uliteketeza nyumba hiyo huku wafanyazi wa kikosi cha zima Moto wakishuhudia tukio hilo bila kuchukua hatua yoyote baada ya gari moja lililokuwepo eneo hilo kuishiwa maji kabla ya kuudhibiti moto huo ambapo hadi gari jingine linafika tayari sehemu kubwa ya nyumba hiyo ilikuwa imeteketea kwa moto. Wapangaji wa nyumba hiyo walidai kwamba chanzo cha moto huo ni shoti ya umeme iliyotokea kwenye chumba kimoja ndani ya nyumba hiyo. “ Tumeona moshi mzito kwenye chumba kile cha uani tukajaribu kuzima bila mafanikiwa baada ya kumuuliza mpangaji wa chumba hicho alidai kwamba ni shoti ya umeme" alisema mmoja wa wapangaji hao.

Mwenye nyumba hiyo Anesta Issa alisema nyumba hiyo waliachiwa ulithi na marehemu baba yao mzee lssa ambaye yeye na mkewe tayari wametangulia mbele za haki. "lnauma sana  hii nyumba tumeachiwa ulithi na wazazi wetu ambao wote wawili  walifariki, tuko watatu mimi Moshi na kaka yetu Mohamed ambaye anaishi humu na wakati moto unawaka alikuwa kazini kiwanda cha Tumbaku mimi na mwenzangu Moshi hatuishi hapa tunaishi kwa waume zetu” alisema Anesta huku akitokwa na machozi. alipoulizwa kama nyumba yao ina bima alidai kwamba haina bima













No comments:

Post a Comment