VPL: YANGA v SIMBA LAIVU SUPERSPORT MEI 18!!
MECHI SITA KUONEKANA SUPERSPORT ‘LIVE’ SUPER WEEK!!
TFF YATAKA MAELEZO YA MCHEZAJI KUHUSU RUSHWA
PATA TAARIFA KAMILI:
Release No. 059
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Aprili 8, 2013
MECHI SITA KUONEKANA SUPERSPORT ‘LIVE’ SUPER WEEK
Kituo cha televisheni cha SuperSport cha
Afrika Kusini kitaonesha moja kwa moja mechi sita za Ligi Kuu ya
Vodacom katika Super Week kati ya Aprili 11 na Mei 18 mwaka huu.
Mechi hizo ni kati Azam na African Lyon
itakayochezwa Aprili 11 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu kwenye
Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam. Yanga na Oljoro
JKT ambayo sasa itachezwa Aprili 13 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka
huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Azam na Simba itakayochezwa Aprili 14
mwaka huu badala ya Aprili 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, na mechi kati
ya Coastal Union na JKT Ruvu itakayochezwa Aprili 16 mwaka huu badala ya
Aprili 10 mwaka huu.
Mechi nyingine ya Super Week
itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ni kati ya Mgambo
Shooting na Yanga itakayofanyika Aprili 17 mwaka huu badala ya Aprili 13
mwaka huu.
Pia mechi nyingine itakayooneshwa live
na SuperSport ni kati ya Yanga na Simba itakayofanyika Mei 18 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kutokana na mechi za Super Week, mechi
kati ya Mtibwa Sugar na Oljoro JKT iliyokuwa ichezwe Aprili 13 mwaka huu
sasa itachezwa Aprili 17 mwaka huu Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani
Morogoro.
TFF YATAKA MAELEZO YA MCHEZAJI KUHUSU RUSHWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limemtaka mshambuliaji Nsa Job wa Coastal Union kuwasilisha
maelezo yake juu ya madai kuwa alipewa rushwa ya sh. milioni mbili ili
asiifunge moja ya timu vigogo vya soka nchini.
Job alikaririwa Aprili 3 mwaka huu na
kituo cha redio cha Clouds FM katika kipindi cha Amplifier kuwa alipewa
kiasi hicho cha fedha na kiongozi wa timu husika ili asiifunge katika
mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom, lakini alipokea fedha hizo na kuifunga
timu hiyo.
Baadaye kiongozi huyo alikuwa akimtaka
arejeshe fedha hizo. Pia TFF imekiandikia kituo hicho cha redio kutaka
nakala ya kipindi hicho ili pamoja na maelezo ya mshambuliaji huyo
vipelekwe katika Kamati ya Nidhamu kwa ajili ya hatua za kinidhamu.
TFF itachukua hatua kali dhidi ya Job
iwapo hatawasilisha maelezo yake kuhusiana na suala hilo, na imetaka
wadau kutoa ushirikiano ili iweze kupambana kikamilifu na vitendo vya
rushwa kwenye mpira wa miguu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment