BM BARBERSHOP KINONDONI

Thursday, April 11, 2013

MADUDU YA LIGI KUU YA BARA PART II,TFF YAVUNJA KANUNI ILIYOTUNGA ILI KUONYESHA MECHI LIVE



MAPEMA wiki hii, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Kamati ya Ligi kwa pamoja walitangaza kuahirisha baadhi ya mechi za Ligi Kuu ya Bara ili kutoa nafasi kwa kituo cha luninga cha SuperSport cha Afrika Kusini kuweza kuonyesha live baadhi ya mechi hizo.

SuperSport kupitia kampeni yake maalum iitwayo SUPER WEEK, itaonyesha mechi hizo katika kile kinachoelezwa kuwa ni kuitangaza Ligi Kuu ya Bara duniani kote. Mechi zilizoahirishwa ni mchezo namba 127, ulipangwa kuzikutanisha Azam FC na African Lyon ambao ulipangwa kuchezwa jana kwenye Uwanja wa Chamazi, mechi hii sasa itachezwa leo Alhamisi 11 Aprili kwenye uwanja huo na itaonyeshwa live.

Mchezo mwingine ni ule namba 156 wa 10 Aprili, mwaka huu kati ya Yanga na JKT Oljoro ambao sasa utachezwa Jumamosi ya 13 Aprili, mwaka huu ili kuipa nafasi SuperSport kuonyesha live mechi hiyo. Pia mchezo namba 155 kati ya Azam na Simba sasa utachezwa 14 Aprili badala ya 13 Aprili mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kama ilivyo kwa Yanga.
Ikumbukwe hii ni zaidi ya mara mbili ndani ya kipindi cha misimu miwili, kituo hiki kinafanya hivi BURE huku kikilazimisha kupangua ratiba ya ligi kuu na kuziathiri baadhi ya timu.

TFF, KAMATI YA LIGI WAVUNJA KANUNI YA LIGI NAMBA 9
Kutokana na Yanga kuwa klabu ya kwanza kulalamikia jambo hili, mambo mengi yameweza kuibuka na kubwa zaidi ni TFF na Kamati ya Ligi kuvunja kanuni namba 9 ya Ligi Kuu ya Bara msimu wa 2012/13 inayoelezea mazingira ya kuahirishwa kwa mchezo.
Kanuni ya 9 ya ligi inasema, Mchezo unaweza kuahirishwa kutokana na sababu yoyote kati ya zifuatazo:-
(a)      Endapo timu ya Taifa ina mchezo.
(b)      Endapo timu inashiriki katika mashindano ya Kimataifa na ina muda usiozidi siku sita kufikia mchezo wa Kimataifa;
(c)    Sababu yoyote ya dharura au/ na yenye msingi itakayokubaliwa na TFF.
(d)   Matukio yasiyotarajiwa wala kusababishwa na timu husika.
(e)    Mchezo wowote ulioahirishwa chini ya kipengele 9 (a),(b) na (c) utapangwa tena katika tarehe itakayoamuliwa na TFF isipokuwa kama utaahirishwa chini ya kipengele 9 (d) utachezwa siku inayofuata iwapo ratiba inaruhusu.
(f)     Iwapo mchezo ulishaanza na kuvunjika kwa sababu ya matukio ya dharura yasiotarajiwa wala kusababishwa na timu husika, utapangwa kurudiwa kwa muda uliosalia, mabao yaliyofungwa katika mchezo huo, Kadhalika kadi walizoonyeshwa wachezaji katika mchezo uliovunjika zitaendelea kuhesabika.
(g)   Taarifa ya maombi ya kuahirisha mchezo ni lazima itolewe kwa maandishi si chini ya siku 14 kabla ya siku ya mchezo, isipokuwa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa binadamu.

UKIUKWAJI WA KANUNI ULIOFANYWA NA TFF, KAMATI YA LIGI  KUHUSU KANUNI YA 9.   
Kama kanuni inavyosema kwamba mchezo unaweza kuahirishwa kutokana na sababu yoyote kati ya zifuatazo:-
(a)               Endapo timu ya Taifa ina mchezo.
       UKWELI NI KWAMBA HAKUNA MCHEZO WOWOTE WA TIMU YA TAIFA.

(b)               Endapo timu inashiriki katika mashindano ya Kimataifa na ina muda usiozidi siku sita kufikia mchezo wa Kimataifa; AZAM PEKEE NDIYO INAYOSHIRIKI MICHUANO YA KIMATAIFA NA HAIKUWA NA MCHEZO WIKI HII AMBAO UNGEILAZIMU KUPANGUA RATIBA.
(c)                Sababu yoyote ya dharura au/ na yenye msingi itakayokubaliwa na TFF.
LABDA HII YA SUPERSPORT INGEWEZA KUWA SABABU YA MSINGI YA KUAHIRISHWA KWA MECHI HIZO, ENDAPO MAKUBALIANO YANGEFIKIWA KATI YA KAMATI YA LIGI, KLABU NA TFF YENYEWE. UKWELI NI KWAMBA, KLABU HAZIKUAFIKIANA NDIYO MAANA BAADHI VILABU KAMAYANGA NA AFRICAN LYON  VIMEJITOKEZA KUPINGA WAZI WAZI HAYO MABADILIKO.
(d)               Matukio yasiyotarajiwa wala kusababishwa na timu husika.
HAKUNA MATATIZO YASIYOTARAJIWA AMBAYO YAMEJITOKEZA WALA KUSABABISHWA NA KLABU HUSIKA. HAPA YAWEZA KUWA HALI YA HEWA YAANI MVUA KUBWA AU JAMBO LA KITAIFA LINALOWEZA KUZUIA MIKUSANYIKO.
(e)                Mchezo wowote ulioahirishwa chini ya kipengele 9 (a),(b) na (c) utapangwa tena katika tarehe itakayoamuliwa na TFF isipokuwa kama utaahirishwa chini ya kipengele 9 (d) utachezwa siku inayofuata iwapo ratiba inaruhusu.
HAKUNA KITU KAMA HICHO KINACHOENDANA NA UAHIRISHWAJI HUU WA SASA.
(f)                 Iwapo mchezo ulishaanza na kuvunjika kwa sababu ya matukio ya dharura yasiotarajiwa wala kusababishwa na timu husika, utapangwa kurudiwa kwa muda uliosalia, magoli yaliyofungwa katika mchezo huo, Kadhalika kadi walizoonyeshwa wachezaji katika mchezo uliovunjika zitaendelea kuhesabika.
HAKUNA KITU KAMA HICHO KINACHOENDANA NA UAHIRISHWAJI HUU WA SASA
(g)               Taarifa ya maombi ya kuahirisha mchezo ni lazima itolewe kwa maandishi si chini ya siku 14 kabla ya siku ya mchezo, isipokuwa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa binadamu.
HAPA NDIPO KWENYE UTATA, KWANI TFF KUPITIA MKURUGENZI WAKE WA MASHINDANO, SAAD KAWEMBA ILITOA TAARIFA KWA NJIA YA BARUA PEPE KWENDA KWA WAJUMBE WA KAMATI YA LIGI  KUHUSU KUAHIRISHWA KWA MECHI HIZO IJUMAA ILIYOPITA YA 5 APRILI, 2013 SAA 9:50 ALASIRI. MUDA HUU HAUPO NDANI YA SIKU 14 KABLA YA SIKU YA MCHEZO. HAPA ILIPASWA TFF KUZITAARIFU KLABU JUU YA JAMBO HILI SI CHINI YA 27 MACHI MWAKA HUU.
Jumapili ya 7 Aprili, mwaka huu, saa 1:32 usiku mtendaji mkuu wa kamati ya ligi bwana Silas Mwakibinga alivitumia vilabu taarifa kwa njia ya barua pepe akivisihi vizingatie mabadiliko ya ratiba kutokana na Super Week ambapo Super Sport wataonesha michezo iliyotajwa na Bwana Saad Kawemba. Cha kushangaza kwanini Bwana Mwakibinga hakuitisha kikao cha viongozi wa vilabu na kujadiliana juu ya hayo mabadiliko ya ratiba ikiwa ni pamoja na kuvijulisha ujio mpya wa Super Sport ?
Mbaya zaidi klabu hizo, nyingine zikawa zinaomba nazo safari hii mechi zao zionyeshwe live huku wakijua fika kwa kuonyesha live mechi hizo, SuperSport inajiingizia kiasi kikubwa cha fedha. Kuonyeshwa live kwa mechi hizo, si sababu iliyo nje ya uwezo wa binadamu.

KUTOKANA NA KUTAMBUA HILO, NDIYO MAANA YANGA KUPITIA KATIBU MKUU WAKE, LAWRENCE MWALUSAKO JUMATATU YA WIKI HII AMBAYO ILIKUWA 8 APRILI SAA 3:54 ASUBUHI ILIJIBU E-MAIL YA KAWEMBA KWA KUSEMA HAIWEZI KUCHEZA JUMAMOSI BADALA YA JANA KWA KUWA TAYARI WALISHAFANYA MAANDALIZI YA MCHEZO WA JUMATANO.

Pamoja na Yanga kuwa na haki ya kukataa mechi yao kuahirishwa, bado TFF na Kamati ya Ligi waliendelea kung’ang’ania mabadiliko hayo ili tu kuifurahisha SuperSport na wengine WANAONUFAIKA na maonyesho ya mechi hizo live.

TFF, KAMATI YA LIGI LAO MOJA
Kwa mchakato huu wa kuipa nafasi SuperSport kuonyesha live mechi zake, inaonekana wazi kwamba TFF na Kamati ya Ligi wapo pamoja na hawazipi klabu uhuru wa kuamua mambo yake.
Kwa mfano Yanga imekataa kucheza mechi yake wikiendi badala ya jana, lakini imelazimishwa kucheza siku hiyo huku Kamati ya Ligi ikiwa kimya isiseme lolote kwa kuitetea Yanga au kuweka mambo sawa kidemokrasia.
Inaonekana wazi Kamati ya Ligi ipo kwa kuinufaisha na kuisimamia TFF kufanya jambo lake lolote kwa klabu za ligi kuu bila yenyewe kuhoji hali yoyote ile. Yawezekana Kamati ya Ligi ndiyo kama isiyoweza kuamua jambo lake lolote ndani ya TFF tofauti na kamati nyingine.
Ili mechi ionyeshwe live, ni lazima klabu husika, TFF na Kamati ya Ligi wote wakubaliane kufanya hivyo. Kwa hili la SUPER WEEK mambo hayakuwa hivyo inavyotakiwa.
    
MSIMAMO WETU
Bado tunaendelea kupambana kuhakikisha kanuni zinafuatwa katika kila jambo linalotokea nchini kwani FAIR PLAY ndicho kitu pekee kinachoweza kutuletea maendeleo katika soka.
Kauli kuwa SUPER WEEK inafanyika ili kuitangaza ligi yetu, inapaswa kuachwa na kuitaka SuperSport kulipia matangazo hayo iwe kwa moja kwa moja au kwa udhamini kama inavyofanya Kenya na kwingineko Afrika ambako kuna ligi dhaifu kuliko ya Tanzania Bara.
Tunachokifanya ni kujaribu kuziamsha klabu kufahamu haki zao na kuweza kunufaika nazo, kwani kwa kufanya hivyo timu zinaweza kupata fedha nzuri za maandalizi na kufanya ushiriki wake katika ligi kuwa wenye mafanikio na kutoa ushindani kwa klabu zenye hali nzuri kifedha.

SOURCE NI SHAFFII DAUDA

No comments:

Post a Comment