BM BARBERSHOP KINONDONI

Wednesday, April 10, 2013

RAFIKI SOKONI NI BORA KULIKO PESA MFUKONI... VICTORIA SOUND NA NGOME NJE YA KINONDONI




Wilaya ya Kinondoni ni eneo maarufu ambapo bendi nyingi za Muziki wa Dansi huwa zinakuwa na maskani huko pamoja na kufanya shughuli zake za Muziki na kujiimarisha. FM Accademia utawapata Msasani Club, Twanga Pepeta Utawapata Mango Garden, Extra Bongo Utawapata Sinza Meeda, Acudo Impact Utawapata Msasani Beach, Mapacha Watatu utawapata Coco Beach, Mashujaa Musica Utawapata Business Park. 

Bendi inayokuja kwa kasi Victoria Sound imeamua kupingana na Usemi huu kwa kuwa na maskani nje ya Kinondoni. Huu unaweza ukawa ni mpango mzuri wa kimapinduzi ambao kama utafanikiwa utaondoa ile dhana kuwa katika jiji la Dar es Salaam, Kila eneo lina aina yake ya Burudani. Mfano ni kama ifuatavyo:
Unapozungumzia Bongo Flava-Basi ujue utaipata kwasana pande za TMK kwa maana ya Temeke na Vitongoji vyake japo si kwamba huku kwenye maeneo mengine haipendwi.

Unapozungumzia Taarabu huwezi kuacha kutaja Ilala na Magomeni. Ukitaka Michiriku hutaiacha Mburtahati, Mbagala na Tandale. Muziki wa Dansi Kinondoni ndiyo Home. 

Je Wazo la Bendi Mpya inayokuja kwa Kasi Victoria Sound Chini ya Meneja Abdulfareed Hussein kupiga nje ya Kinondoni kunaweza kuleta TIJA pamoja na kubadilisha mazoea yaliyozoeleka kuwa KINOKINO ndiyo Nyumbani kwa Muziki wa Dansi??Lets Wait

No comments:

Post a Comment