BM BARBERSHOP KINONDONI

Sunday, August 5, 2012

PENGO LA YONDANI KUZIBWA NA GLADYS BOKESE WA DRC CONGO


GLADYS BOKESE
Katika kujaribu kuziba pengo la nafasi ya mlinzi wa kati ambayo imeachwa na mlinzi kitasa Kelvin Yondani maarufu kama VIDIC aliyejiunga na klabu ya Yanga hivi karibuni, mabingwa wa bara Simba SC inakamilisha usajili wa mlinzi wa timu ya taifa ya DRC Congo Gladys Bokese ambaye ni mchezaji huru. Gladys Bokese ambaye alikuwa akiitumikia kwa mara ya mwisho klabu ya Étoile Sportive du Sahel ya Tunisia alitarajiwa kuwasili nchini Tanzania leo hii akitokea nchini Congo tayari kukamilisha taratibu za usajili. Taarifa zilizoifikia Blog ya Mwanatanga zimesema mchezaji huyo alikuwa apokelewe na Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange Kaburu uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere saa 10:00 jioni ya leo.
BOKESE AKISHANGILIA GOLI

Gladys Bokese alizaliwa September 9, 1981 jijini Kinshasa ambako aliaanza kucheza soka akiwa na klabu ya AS Bandal akicheza kama mshambuliaji. Toka Bandal alijiunga na Daring Club Motema Pembe kifupi DC Motema Pembe akiwa na wachezaji kadhaa nyota kama Mbala Mbuta Biscotte na Ngasanya Ilongo. Alianza kuichezea timu ya taifa ya Congo mwaka 2006 na kuwa ni miongoni mwa wachezaji waliounda kikosi kilichoshiriki fainali za mataifa ya Afrika mwaka huo. Alipojiunga na timu ya taifa kocha wa timu ya taifa ya Congo Claude Le Roy alimbadilisha nafasi ya uchezaji na kumtumia kama mlinzi wa kati eneo ambalo amelimudu vema na mpaka sasa akiwa ni mlinzi wa kati tegemeo.
 BOKESE AKIWA KATIKA MAJUKUMU YA KITAIFA

Taarifa za uhakika za mchezaji huyo kuja Tanzania zimethibitishwa na ndugu wa karibu wa mchezaji huyo ambaye amekuwa na mahusiano mazuri na Blogger hii.

No comments:

Post a Comment