BM BARBERSHOP KINONDONI

Sunday, August 5, 2012

WAZIRI GEORGE HURUMA MKUCHIKA ATEULIWA KUINGIA KWENYE BARAZA LA WADHAMINI LA YANGA


Kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga iliyokutana leo 05/08/2012 Makao makuu ya klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake Yusufu Mehboob Manji imemtangaza Mheshimiwa George Huruma Mkuchika kuwa mmoja wa wajumbe wa baraza la wadhamni wa klabu hiyo. Sambamba na Mkuchika wengine waliochaguliwa ni pamoja na Seif Ahmed Magari, Ammi Mpungwe, Isaack Chanji na Mohamed Nyengi amewateua kuingia katika kamati ya utendaji huku jina moja likitafutwa kwa ajili ya kukamilisha idadi kamili ya wajumbe wa kamati ya utendaji.

Uamuzi huo umetolewa na mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji katika mkutano wa kusimikwa rasmi madarakani kwa uongozi mpya wa klabu hiyo leo makao makuu ya klabu hiyo chini ya mama mlezi wa Yanga mama Fatma Karume. Sambamba na uteuzi wa kamati hiyo mpya ya utendaji, klabu hiyo pia imeamua kufutilia mbali kamati zote ndogondogo ndani ya klabu hiyo kuanzia leo isipokuwa kamati ya uchaguzi inayoongozwa na Mheshimiwa Jaji John Mkwawa.

Katika kuhakikisha kunakuwepo na umoja zaidi ndani ya Yanga wakati wa maamuzi, uongozi wa Yanga umesema utakuwa ukikutana na viongozi wa matawi kila mwezi kwa lengo la kubadilishana mawazo. Katika mkutano wa kusimikwa kwa viongozi hao wapya wa klabu viongozi wote wapya walikuwepo na kuapishwa na mwenyekiti wa baraza la wazee Mzee Ibrahim Katundu  isipokuwa mjumbe mmoja ndugu Abdalah Bin Kleb ambaye yuko Kigali Rwanda akishughulikia masuala ya klabu ya Yanga. Katika hatua nyingine mwenyekiti wa klabu hiyo Bwana Yusufu Manji amesema wanatarajia kufanya sherehe ya kuchukua taji la Kagame baada ya mfungo wa mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani.

No comments:

Post a Comment