Wafanyakazi
wa hospitali ya seliani wakiwa wanamuhamisha hospitali mtoto huyo
baada yakukosa kifaa cha kumpimia katika hospitali hiyo na kumpeleka
hospitali ya agakan
|
JESHI la
Polisi Mkoani Manyara limeingia katika shutuma nzito baada ya Askari wake watatu
kutuhumiwa kumpiga mtoto mwenye umri wa miaka 16 wa jamii ya kifugaji
anayejulikana kwa jina la Kadogoo Kalanga mkazi wa Orkesmet Wilayani Simanjiro
hadi kupoteza fahamu.
Tukio
hilo lilitokea Jumatatu Agosti 28, 2012 majira ya saa tano na nusu katika
eneo la Orkesmet ambapo askari watatu mmoja wao akitambulika kwa jina moja tu
la John walimkamata mtoto huyo mara baada ya kumtuhumu kuiba mbuzi wa jirani
yake ambaye anajulikana kama Mama Shedi mkazi wa eneo hilo la Orkesmet.
Mashuhuda
wanadai kuwa polisi hao baada ya kumkamata mtoto huyo, walianza kumuadhibu bila
huruma, Wamshambulia kwa marungu na
kumbana sehemu zake za siri hadi kutokwa na haja ndogo na baadaye alipoteza fahamu. Hali hiyo ilipelekea mtoto huyo kulazwa katika kukimbizwa
hospitali ya Orkesmet lakini Wauguzi wa hapo walishauri akimbizwe hospitali ya
Mkoa. Kwasasa motto huyo amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) katika
Hospitali ya Selian iliyopo jijini Arusha.
Mama
mzazi wa kijana kadogoo kalanga ambaye alipigwa na maaskari wa kituo cha
olkesimeti akiwa anaonyesha sehemu ambazo mtoto wake anamaumivu makali
baada ya kupigwa
|
Uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa hakuna jarida lolote lililofunguliwa kutokana na kisa
hiki. Watu wakaribu na mtoto huyu wanadai kuwa walitaka kufungua mashtaka dhidi
ya askari waliofanya unyama huo lakini walikataliwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari nje ya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) ndani ya
Hospitali ya Selian mama mzazi wa kijana huyo, Bi. Paulina Kalanga
alisema kwamba askari hao watatu walimfuata kijana wake eneo la mnadani na
kumtuhumu kuiba mbuzi na kuanza kumshambulia kwa kumpiga bila kumpa nafasi ya
kujitetea kitendo kilichopelekea kuanza kutokwa na haja ndogo mfululizo na
kisha kupoteza fahamu.
“Yaani
walimkamata kijana wangu kisha wakaanza kumpiga kwa marungu na mateke …..
wakazishika sehemu zake za siri na kuanza kugongagonga na kitako cha silaha ya
moto ndipo alipoanza kujikojolea mfululizo na kupoteza fahamu”alisema huku
machozi yakimtiririka Taarifa
zinasema kuwa polisi hao baada ya kuona hali ya mtoto huyo imekuwa mbaya
walimbeba na kisha kumkimkimbiza haraka katika kituo cha afya cha Orkesmet kwa
ajili ya matibabu kabla wanandugu kuomba gari la wagonjwa mahututi (ambulance)
kumkimbiza katika hospitali ya Selian iliyopo mkoani Arusha.
Majeruhi Kadogoo Kalanga(16)mkazi wa Orkesmet akipatiwa huduma |
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoani Manyara, Akili Mpwapwa alipohojiwa juu ya tukio hilo
alikiri kupata taarifa zake huku akisema kwa kifupi kwamba tayari
ameshatoa maelekezo kwa mkuu wa polisi wilayani humo kufanya uchunguzi wa kina
juu ya tukio hilo na kisha aletewe ripoti kamili mezani kwake.
No comments:
Post a Comment