Mkazi
wa Ndembezi mjini Shinyanga amepigwa na mumewe hadi kuzirai na kukimbizwa
hospitalini kwa matibabu baada ya kutoa ushirikiano kwa karani wa Sensa ya Watu
na Makazi. Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Evarist Mangala, alisema kuwa
mwanamke huyo, Esther Zablon (40) alipigwa juzi saa mbili asubuhi baada ya
mumewe, Ismail Yahya kupata taarifa kuwa karani wa sensa alifika nyumbani kwao
na mkewe kukubali kuhesabiwa na kutoa takwimu za familia yao.
Akisimulia,
Kamanda Mangala alisema karani huyo alipokwenda nyumbani hapo, mume hakuwapo na
kama mkuu wa kaya, Esther akazungumza na kutoa taarifa. Alisema baada ya mume
kurudi nyumbani na kugundua kuwa mkewe alikubali kuhesabiwa, alimshambulia kwa
ngumi na mateke na kusababisha mke huyo kupoteza fahamu.
Kutokana
na kipigo hicho, kwa mujibu wa Kamanda Mangala, Esther alikimbizwa katika
Hospitali ya Mkoa kwa uchunguzi na matibabu. "Wakati mwanamke huyo
akichukua fomu namba tatu ya Polisi (PF3) kituoni kabla ya kufikishwa
hospitalini, huku akilia kuwa sababu ya kipigo ni yeye kukubali kuhesabiwa,
jambo ambalo ni kinyume na msimamo wa dini ya mumewe (Uislamu)," alisema
Kamanda Mangala.
Hata
hivyo, Kamanda alisema Esther alitoroka wodini kwa kuhofia mumewe kukamatwa na
hatimaye kufungwa. Kamanda Mangala alisema Polisi wanaendelea kumtafuta Yahya
na akipatikana atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili.
Inaelekea sheikh Issa Ponda amefanikiwa kuanzisha madhehebu ya kiislamu inayokataza wafuasi wake kuhesabiwa. Huyo ndio kinara wa mtandao wa kupinga sensa na mamlaka zinafahamu ila wanamgwaya. Au mnasubiri hadi awe Aboud Robo wetu. Watu wanaohujumu dola kwa pazia la dini wasionewe aibu watakuja kutuletea janga.
ReplyDelete