*Kichwa cha ng'ombe.
*Kiwiliwili cha binadamu.
Na Ezekiel Kamanga,Chunya.
Mwanamke mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Shija
Paulo(35),mkazi wa Kijiji cha Magaga,Kata ya Mbuyuni Wilaya ya Chunya Mkoani
Mbeya amejifungua kiumbe kinachofanana na ng'ombe chenye jinsi ya kiume.
Tukio hilo limetokea Septemba 16 mwaka huu majira ya saa 11
alfajiri,mwanamke huyo alipokuwa amepelekwa katika Zahanati ya Mbuyuni kwa
ajili ya kujifungua akiwa na mumewake Bwana Mwigulu Yangula(Makeni) lakini
kabla ya kufika zahanati mwanamke huyo alipatwa na uchungu ndipo alipoomba
msaada kwa Mkunga wa jadi aliyekuwa karibu Bi. Agripina Fredrick
Sikanyika(Namwinje).
Mkunga huyo alimpokea mwanamke huyo na kujifungua salama huku
kiumbe hicho kikiwa na kichwa na domo mithili ya ndama(mtoto wa ng'ombe) chenye
dalili ya kuota mapembe na manyoya meusi hadi eneo la kifuani ambapo kutoka
hapo kifuani mpaka miguuni alikuwa na umbile la binadamu na jinsi ya
kiume licha ya kutimiza miezi tisha ya kuzaliwa na uzito wa wastani.
Hali hiyo ilimtisha sana Mkunga Bi. Sikanyika na kuitwa Bwana
Yangula kushuhudia kiumbe hicho naye alistaajabu kwa yale yaliyotokea.
Hata hivyo kiumbe hicho kilidumu kwa muda wa masaa matatu
na kufariki dunia na katika uchunguzi wa mwandishi wa habari hii amebaini kuwa
hiyo ilikuwa ni mimba ya nane kwa mwanamke huyo na kila mimba hupata watoto
ambao si riziki.
Tukio hilo pia lilishuhudiwa na mhudumu wa Kituo cha
Afya,kitongoji cha Magaga Bwana Josephat Alisen Ismail,ambaye naye amesema
ameshangazwa na tukio hilo na kusema hajawahi kukutana na jambo hilo katika taaluma
hiyo ya utabibu.
Wakati wa tukio hilo Afisa Mtendaji wa Kijiji Bwana Michael
Sanziwa hakuwepo na alipopigiwa simu aliruhusu kiumbe hicho kichukuliwe na
mzazi ambapo maziko yake yalifanyika kandokando ya nyumba ya Bwana Yangula.
Katika tukio hilo watu wengine wamelihusisha na imani za
kishirikina na wataalamu wa viumbe wamesema kuwa mara nyingi viumbe hivyo huwa
haviishi muda mrefu,lakini hali ya mama aliyejifungua inaendelea vema baada ya
kujifungua.
No comments:
Post a Comment