BM BARBERSHOP KINONDONI

Saturday, September 8, 2012

BAHANUZI SPIDER MAN ACHAFULIWA MTANDAONI FACEBOOK


MSHAMBULIAJI hatari wa Timu ya Yanga aliye kwenye chati kwa sasa, Said Bahanuzi amefanyiwa kitu mbaya katika mtandao wa kijamii maarufu kama Facebook. Mwanandinga huyo alipatwa na masahibu hayo kufuatia mtu asiyejulikana kufungua akaunti kwa kutumia jina la straika huyo hatari na kuanza kuwasiliana na watu mbalimbali ambapo wengi walikuwa wakiamini wanawasiliana na Bahanuzi.

Akichezesha taya na Udaku Spoti, Bahanuzi alisema hajawahi kujihusisha na masuala ya Facebook na kusema hajui lolote juu ya mtandao huo lakini amemlaani vikali mtu huyo anajifanya ni Bahanuzi kwani anamchafulia.

No comments:

Post a Comment