BM BARBERSHOP KINONDONI

Saturday, September 8, 2012

PINDA ATIMUA WAKURUGENZI 5 MMOJA AOMBA KUPUMZIKA ATEUA 13 WAPYA AHAMISHA 27 SABA AWAPA UKAIMU


WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO KAYANZA PETER PINDA
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewavua madaraka Wakurugenzi sita wa Halmashauri nchini, kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo udhaifu katika kutekeleza majukumu yao. Uamuzi huo ulitangazwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia aliyeonya kuwa, Waziri Mkuu hatasita kuendelea kuwachukulia hatua watumishi watakaoshindwa kuwajibika.
WAZIRI WA TAMISEMI MHE. HAWA GHASIA
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Hawa Ghasia aliwataja waliovuliwa madaraka na Waziri Mkuu kuwa ni pamoja na
1.      Mpangalukela Tatala (Geita) na Theonest Nyamhanga (Kishapu), ambao sababu za kuvuliwa kwao madaraka zimetajwa kuwa ni kushindwa kusimamia rasilimali watu na fedha. Aidha,
2.      Eden Munisi (Morogoro) ameondolewa kutokana na kuisababishia halmashauri yake kupata hati chafu, kushindwa kusimamia rasilimali watu na uzembe. Wengine,
3.      Mhando Senyangwa (Kyela) ana kesi mahakamani wakati
4.      Nicholaus Kileka (Ngorongoro) alikuwa na kesi iliyoendeshwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), wakati mmoja,
5.      Willy Njau (Mwanga), ameomba kuachwa katika nafasi yake kutokana na sababu za kiafya.
Waziri Ghasia ameongeza kuwa “Michakato ya kinidhamu inaendelea na baadhi yao tayari wana kesi mahakamani na wengine tumeshawafikisha TAKUKURU, na kwa sasa TAMISEMI tumejipanga vizuri, tutawachukulia hatua za kinidhamu watumishi wote ambao hawawajibiki ipasavyo,” alisema Ghasia. Wakati hao wakisimamishwa kazi, Serikali imetangaza
Majina ya Wakurugenzi wapya walioteuliwa kujaza nafasi hizo kuwa ni pamoja na Halmashauri zao katika mabano ni:
  1.  Naomi Nko (Magu)
  2. Mohammed Maje (Namtumbo)
  3. Abdallah Mfaume (Kyela)
  4. Adam Mgoyi (Mbarali)
  5. Estomih Chang’a (Mpanda)
  6. Leti Shuma (Mwanga)
  7. Fulgency Mponji (Moshi)
  8. Robert Nehata (Tunduru)
  9. Isabela O. Chilumba (Kahama)
  10. Isabela D. Chilumba (Ulanga)
  11. Fikiri Malembeka (Sengerema)
  12. Nassib Mbaga (Biharamulo)
  13. Jovin Jungu (Chamwino)
Waziri pia amewahamisha Wakurugenzi 27 kutoka vituo vyao vya kazi. Majina na sehemu wanazotoka zikiwa kwenye mabano ni:
  1. Bibie Mnyamagola, Kongwa (Kilindi)
  2. Daudi Mayeji, Kilindi (Chamwino) 
  3. Protace Magayane, Nkasi (Igunga), 
  4. Saada Mwaruka, Mkuranga (Nkasi)
  5. Sipora Liana, Tabora (Mkuranga)
  6. Hadija Makuwani, Tabora (Tabora Manispaa)
  7. Doroth Anatoli, Kasulu (Tabora)
  8. Kelvin Makonda, Lindi (Kasulu)
  9. Pudenciana Kisaka, Iringa (Ulanga)
  10. Tina Sekambo, Makambako (Iringa)
  11. Beatrice Dominic, Masasi (Bukoba)
  12. Gladyness Ndyamvuye, Bukoba (Masasi)
  13. Nathan Mshana, Ngorongoro (Musoma)
  14. Cornel Ngudungi, Ngara (Magu) 
  15. Mohammed Mkupete, Mtwara (Njombe)
  16. Koroine Ole Kuney, Misungwi (Ngorongoro)
  17. Ephraim Ole Nguyaine, Rorya (Tunduru)
  18. Goody Pamba, Igunga (Hanang)
  19. Fidelis Lumato, Ludewa (Tarime)
  20. Athuman O, Tarime (Kongwa)
  21. Ahmad Sawa, Musoma (Lindi)

WAFUATAO NI WAKURUGENZI WANAOHAMISHWA KWENDA HALMASHAURI MPYA:
  1. Magreth Nakainga, Geita (Mtwara)
  2. Eliza Bwana, Bariadi (Kahama)
  3. Zuberi Mbyana, Ilemela (Biharamulo)
  4. Mohammed Nanyanje, Masasi (Sumbawanga)
  5. Erica Musika, Kahama (Sengerema)
  6. Imelda Ishuza, Busokelo (Makete) 
 WALIOTEULIWA KUKAIMU NI ;
  1. Abdallah Kidwanka (Geita)
  2. Rutius Bilakwata (Kishapu)
  3. Twalib Mbasha (Monduli)
  4. Henry Rugayu (Urambo)
  5. Iddi Nganya (Makete)
  6. Paul Malala (Njombe)
  7. Felix Mabula (Hanang)

No comments:

Post a Comment