Kihistoria Mkoa wa Tanga
ulitumiwa sana na wakoloni wa Kireno, Kiarabu, Kijerumani na Kiingereza ikiwa
lango la biashara na uchumi kwa kuunganisha sehemu za ndani za Afrika Mashariki
na Kati na sehemu mbalimbali za Dunia kupitia
bahari ya Hindi. Mwaka 1840 eneo la Manga lilikuwa njia
waliopitia wafanyabiashara kutoka Bara Arabu
waliokuja kutafuta meno ya tembo na watumwa. Waarabu walikuwa
wakiacha vyombo vya usafiri (majahazi) eneo la Sadani (Bagamoyo) na kuanza
safari kupitia Manga, Kimbe hadi Kondoa Irangi. Misafara mingine ya
wafanyabiashara ilianzia Unguja kupitia Pangani, Kiwanda (Sindeni),
Ngugwini, Mbego, Kwediboma, Mgera hadi Kondoa Irangi ambapo walileta nguo,
shanga na vitu ili kubadilishana na pembe za ndovu,
watumwa, chakula na mifungo. Kutokana na mwingiliano wa tamaduni mbalimbali,
wenyeji wa Tanga wamerithi tamaduni, lugha na ustaarabu wa mataifa
mbalimbali ya Washirazi, Waarabu, Wachina, Wahindi, Wareno,
Wajerumani, Waingereza na Waswahili.
Mkoa wa Tanga ni
mzizi na chimbuko la Tanganyika kabla ya kuungana na visiwa vya Unguja na Pemba
mwaka 1964 na kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Tanganyika ilipata Uhuru
mwaka 1961 huku Mkoa wa Tanga ukiwa ni msafirishaji mkubwa wa zao la Mkonge
duniani na mhimili wa kukua kwa uchumi wa
nchi. Jina Tanga lilitolewa na wafanyabiashara
wa Kishirazi likiwa na maana nne ambazo
ni Tambarare, Mabonde ya Kijani, Barabara za Milimani
na Kilimo cha Milimani. Neno nyika ni la kibantu ambalo lilikuwa
likitumiwa sana na wenyeji wakimaanisha mbuga au pori zaidi ya jina Tanga.
Harakati za kudai
Uhuru kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza zilifanikiwa na Tanganyika kupata
Uhuru tarehe 9 Disemba, 1961 chini ya uongozi wa Hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere ndani ya chama cha TANU. Wakati huo (1961) Mkoa wa Tanga
ulikuwa ni Jimbo lenye Wilaya tano (5) ambazo ni Wilaya ya Tanga, Handeni,
Pangani, Usambara na Same.
Mkoa wa Tanga kwasasa
una Wilaya … ambazo ni pamoja na Tanga Mjini, Tanga Vijijini, Muheza, Pangani,
Mkinga, Korogwe, Handeni, Kilindi na Lushoto
Chanzo cha habari hii
ni: Tanzania Regions Site
ENEO LA RASKAZONE TANGA-HII NDIYO MASAKI YA TANGA |
UWANJA WA NDEGE WA TANGA |
No comments:
Post a Comment