Wanachama wa CUF Kata ya Msambweni Jijini Tanga waliamua
kutumia jeneza bandia na kinyago cha maiti kuonyesha hisia zao za
kufurahia ushindi wa Kata hiyo waliyoupata kwenye uchaguzi uliofanyika kwenye
kata hiyo. Kitendo hiki cha Wanachama wa CUF kata ya Msambweni
mjini Tanga sidhani kama ni kizuri cha kuweza kusimma mbele ya
Umati au Umma wa watu na kukifurahia kwa kuwa tunafanya DHIHAKA ambao
zinatupeleka Kubaya.
Ushabiki wa namna hii unaweza kuleta chuki na madhara
baina ya jamii. Ni haki yao CUF kuonyesha furaha yao ila kwa jinsi hii
haipendezi! kuweka picha ya mgombea wa CCM Ndugu Godfrey Mazimu aliyeshindwa
kwenye uchaguzi kwenye mfano wa jeneza bandia tena huku wakiweka sanamu ambayo
kila anae pita njia anatupia pesa kama rambirambi haipendezi na
sidhani kama ushabiki huu unafundisha kitu.
Laah, hii inaonyesha watu walivyochoka CCM. Vita ya kuwaondoa mafisadi mstari wa mbele wa chama wamesarenda. Nape na wale waliotegemewa na wanaCCM halisia wamebaki domokaya ujasiri hakuna. WanaCCM wa kweli wamenyang'anywa chama na mafisadi, lao hakuna... Hakuna tena cha ahadi ya mwanachama, imani wala cha itikadi, ni biashara haramu tu... Uuuuuuuwiiiii, tumekwisha.
ReplyDelete