BM BARBERSHOP KINONDONI

Sunday, September 23, 2012

DHIHAKA HII YA CUF TANGA IMEPITILIZA


Wanachama wa CUF Kata ya Msambweni Jijini Tanga waliamua kutumia jeneza bandia na kinyago cha maiti kuonyesha hisia zao za kufurahia ushindi wa Kata hiyo waliyoupata kwenye uchaguzi uliofanyika kwenye kata hiyo. Kitendo hiki cha Wanachama wa CUF kata ya Msambweni  mjini Tanga  sidhani kama ni kizuri cha kuweza kusimma mbele ya Umati au Umma wa watu na kukifurahia kwa kuwa tunafanya DHIHAKA ambao zinatupeleka Kubaya. 

Ushabiki wa namna hii unaweza kuleta chuki na madhara baina ya jamii. Ni haki yao CUF kuonyesha  furaha yao ila kwa jinsi hii haipendezi! kuweka picha ya mgombea wa CCM Ndugu Godfrey Mazimu aliyeshindwa kwenye uchaguzi kwenye mfano wa jeneza bandia tena huku wakiweka sanamu ambayo kila anae pita njia anatupia pesa kama rambirambi  haipendezi na sidhani kama ushabiki huu unafundisha kitu.

1 comment:

  1. Laah, hii inaonyesha watu walivyochoka CCM. Vita ya kuwaondoa mafisadi mstari wa mbele wa chama wamesarenda. Nape na wale waliotegemewa na wanaCCM halisia wamebaki domokaya ujasiri hakuna. WanaCCM wa kweli wamenyang'anywa chama na mafisadi, lao hakuna... Hakuna tena cha ahadi ya mwanachama, imani wala cha itikadi, ni biashara haramu tu... Uuuuuuuwiiiii, tumekwisha.

    ReplyDelete