NGUZA MBANGU MASHINE NDANI YA MJENGO WAKE |
Mtoto wa Mwanamuziki Nguli Mzee Nguza (Babu Seya) ambaye alikuwa Mpiga Drum Maarufu ambaye mimi namuita ambaye hajawahi kutokea ndani ya FM Accademia kwa miongo kadhaa sasa Nguza Mbangu Mashine ameonyesha mfano kwa Wanamuziki wengine kuwa ukiwa na nia inawezekana baada ya kujikwamua na Kujenga Bangaloo maeneo ya Mbezi Luis Dar es Salaam kwa ushirikiano na Mke wake Hilda Kibwana.
Akiongea na mwanatanga Nguza alisema kuwa baada ya kurejea toka Kifungoni kwanza alimkabidhi Mungu maisha yake, pili akaungana na Mkewe na tatu wote kwa pamoja wakajipanga na kuanza kupigana na maisha ili kujikwamua. Mwanzo ilikuwa ni kazi ngumu sana lakini kwa kuwa mungu alikuwa nao daima hatimaye wameweza kujenga Jumba lao hilo ambalo sasa limekamilika na maisha yanaendelea.
Nguza na Hilda wanaamini kuwa hakuna lisilowezekana chini ya jua hili la Mungu. Wao wameweza wanaamini kuwa hata wengine wataweza kama wao kubwa ni kujituma bila kujali kama kuchoka lakini ukiwa umemtanguliza Mungu.
Mwanatanga blog inaamini kuwa wanamuziki hupata pesa nyingi sana lakini
wanakosa mipango. Nguza ameaonyesha mfano na nyinyi igeni .. mambo haya
si ULOZI bali ni bidii na kujituma bila kuchoka huku mipango ikichukua
nafasi yake. Hongera Nguza kwa kuonyesha Mfano. ACHENI KULALAMA KWA
KISINGIZIO CHA MASLAHI INAWEZEKANA
NGUZA AKIWA UANI KWA MJENGO WAKE |
HILDA KIBWANA MKE WA NGUZA AKIFANYA UKAGUZI WA MJENGO WAO |
MUONEKANO WA NYUMBA YA NGUZA KWENYE MLANGO MKUBWA WA KUINGILIA |
HILDA KIBWANA AU MRS. NGUZA |
MJENGO WA NGUZA KWA NYUMBA |
MKE WA NGUZA (HILDA KIBWANA AKIFANYA UKAGUZI WA PAVEMENT BLOCKS |
NGUZA NDANI YA SEBULE KWA KUJIDAI |
MDOGO WAKE NGUZA MASHINE |
NGUZA NDANI YA MJENGO |
NGUZA NDANI YA CORRIDOR MJENGONI |
KALUNINGA FLAT KWA MBAAAALI |
KUSALI NI SEHEMU KUBWA YA MAISHA YA NGUZA MASHINE |
NGUZA KATOKEZEA AU??? |
NGUZA |
NGUZA |
HILDA KIBWANA (MRS. NGUZA) KWENYE POZI |
MR & MRS NGUZA MBANGU MASHINE |
No comments:
Post a Comment