Mkazi
wa mtaa wa Mpanda hotel wilaya yam panda mkoa wa katavi Nzego Vicent (33)
amejiua kwa kujinyonga na kamba baada ya mkewe kumnyima tendo la
ndoa. Tukio hilo limetokea hapo juzi majira ya saa 7:30 usiku jirani na nyumba
waliokuwa wakiishi wanandoa hao. Mke
wa marehemu huyo aitwaye Agnes Nicodemu alisema siku hiyo ya tukio hilo mumewe
ambaye alikuwa ametoka kwenye pombe za kienyeji alifika nyumbani kwake majira
ya saa 6:20 usiku na kumtaka mkewe ampe tendo la ndoa. Alisema
kutokana na shughuli alizokuwa amezifanya mchana alimwomba mumewe avumilie hadi
siku itakayofuata kwa kile alichomweleza kuwa hakuwa tayari kufanya nae tendo
landoa kwa kuwa alikuwa amechoka.
Baada
ya marehemu Nzego kujibiwa hivyo hakuridhika nna kauli hiyo ya mkewe na ndipo
alipoanza kumshutumu kuwa huenda ana mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine.
Ndipo Nzego alipoamua kuanza kumshambulia mkewe huyo kwa kumpiga kichapo huku
akimtolea maneno ya kumtisha kuwa lazima atamuua kwa panga. Agnes baada ya
kuona kipigo kimezidi aliamua kukimbia nje ili kukwepa kipigo alicho kuwa
akichapwa na mumewe.
Baada
ya mkewe kukimbia marehemu aliamua kutoka nje huku akiwa na shoka mbili na
kuelekea kusiko julikana na kuacha nyumba yake ikiwa wazi. Ndipo majira ya ssa
12:30 asubuhi mkewe na marehemu alipofuatwa na majirani na walimweleza kuwa
mumewe amejinyonga kwa katani jirani na nyumba waliyokuwa wakiishi. Mkewe huyo
aliamua kufuatana na majirani hao hadi kwenye eneo hilo na ndipo alipomwona
mumewe akiwa amening’inia juu ya mti akiwa amekata roho. Kamanda wa polisi mkoa
wa katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutokea kwa kifo hicho cha mtu
kujinyonga kwa kutumia kamba katika mtaa huo
No comments:
Post a Comment