Mwandishi wetu, Serengeti-Mara
ASKARI magereza wa gereza la mahabusu lililoko mjini Mugumu wilayani Serengeti Mkoani Mara mwenye namba B.6262 WDR Alphonce Mayuma(21)amejiua kwa kujipiga risasi mdomoni na kutokea kisogoni wakati akiwa kwenye lindo. Mganga mkuu wa hospitali teule ya Nyerere DDH Dk.Calvin Mwasha amesema mwili wa askari huyo umefikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa uchunguzi na kubaini aliumizwa na kitu chenye ncha kali kilichoingilia mdomoni na kutokea kisogoni.
Baadhi ya askari wakiongea na Redio Free Afrika kwa sharti la kutotajwa majina wamesema chanzo ni kutakiwa kuandika maelezo kufuatia tukio la kumwibia mwenzake tsh220,000 kupitia Mpesa. Kosa alilokiri mbele ya uongozi wa gereza hilo na kulipa lakini alipoambiwa kuandika maelezo alionekana kutokukubaliana kwa madai kuwa walikusudia kumfukuza kazi na siku iliyofuata ndipo akajilipua wakati yuko zamu. Mayuma ambaye ameajiriwa mwaka 2010 amekufa hajamaliza mkataba wa miaka mitatu ya awali ,mwili wake unasafirishwa kwenda kwao mkoani Shinyanga kwa ajili ya maziko.
No comments:
Post a Comment