BM BARBERSHOP KINONDONI

Friday, October 12, 2012

TWANGA FACEBOOK FANS PARTY KWA AJILI YA SHUKURANI HII HAPA

Bendi maarufu nchini inayopiga miziki ya Dansi kwa miongo zaidi ya kumi na mbili sasa Twanga Pepeta SUGU imeandaa onyesho maalum kwa ajili ya Wapenzi wake wa nje na ndani ya Dar es Salaam na Afrika kwa ujumla wake siku ya Jumapili Tarehe 21/10/2012 katika ukumbi wa Kistaarabu wa Mzalendo Pub juu ya Jengo la Kisasa la Milenium Tower. Unakula Muziki wa Dansi huku ukiwachungulia wengine kwa chini.
Onyesho hili ni lililobatizwa jina la TWANGA FACEBOOK FANS PARTY limeandaliwa MAALUM kabisa kwa ajili ya kuwakutanisha wadau wa Mitandao mbalimbali kama vile, Blogs, Websites, Followers, Facebook, Twitter, BBM, What's Up na wale wote ambao wamekuwa wakitoa Mchango wao mkubwa kwa Bendi ya Twanga Pepeta na Bendi nyingine za Dansi kwa miongo mingi katika Dunia hii ya Utandawazi kupitia Technologia hii maarufu sasa kote Duniani. Katika onyesho hili maalum wadau wote wenye account ndani ya Facebook, Twitter, Blogs, Website wanaalikwa kuhudhuria onyesho hili maalum kabisa litakalo kuwa la aina yake na pekee kwa miongo mingi sasa.
Katika Onyesho hilo wamealikwa wanamuziki wote ambao wamewahi kupitia ndani ya Bendi ya Twanga Pepeta Tangu Kisa cha Mpemba hadi sasa Shamba la Twanga. Nyimbo mbalimbali ambazo ziliwahi kupigwa kwenye kila albam zitaimbwa na wahusika kuanzia kwenye upigaji vyombo hadi kwenye Muziki na ghani za RAP kama vile Kutesa kwa zamu, Piga Bao, Kidali Po, Mugongomugongo, Shabani Madobe, Mwajuma Ndalandefu, Timbwili la Asha Ngedere, Mama Vanesa, Kisigino, Njegere kwa Ubwabwa, Watu wazima Hovyo hawana lolote, nasasa RAP inayobamba ya WASUUUTE.
Kutakuwa pia na Nyama Choma maalum kabisa kwa wadau wote watakaoingia Ukumbini siku hiyo mapema kuanzia saa tatu hadi saa tano .
Siku hiyo pia zitatolewa Certificate kwa wadau mbalimbali wa Mitandao hiyo ya Kijamii kwa kila njanja ili kuonyesha kukubali mchango wa eneo hili Muhimu la uhamasishaji na uelimishaji wa jamii kwenye suala la Muziki wa Dansi.
Pia siku hiyo kutakuwa na utambulisho wa MABALOZI wawili wa Twanga Pepeta kwa jinsia ya Kike na kiume ambao watakuwa wanabeba ujumbe mzito wa kuitangaza Twanga Pepeta wanapokuwa kwenye Shughuli mbalimbali za Kitaifa Nje na ndani ya Tanzania kwa misingi ya Kubadilisha uelekeo kwenye Tasnia hii Muhimu kwa misingi ya kuirejesha ilikotoka baada ya kuingiliwa na Wadau ambao huenda wanakusudia kujenga au kinyume chake.
Viingilio vitakuwa vya kawaida sana ambavyo kila mdau atamudu kwa maana ya shilingi 5000/= kwa kila kichwa kwakuwa bendi yako inakujali wewe Mtanzania unayeisapoti bendi yako kila kukicha.
Wahi tiketi yako sasa Ofisi za ASET kinondoni.

No comments:

Post a Comment