Timu ya Tanzania Prison
ya Mbeya imepata ajali mbaya eneo la Hale Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga. Ajali hiyo imetokea baada ya gari walilokuwa wakitumia aina ya Coaster kupigwa na mwanga mkali wa taa za Gari walilokuwa wakipishana nalo na dereva kushindwa kuona mbele na kusababisha gari kupotea njia na kupinduka. Taarifa hizi zimetolewa na Kiungo wa timu hiyo ndugu Diego Magai.
No comments:
Post a Comment