Handaki
la ajabu limeonekana katika eneo la kata ya kitanzini mtaa wa sokoni mjini
Iringa. Katika tukio hilo lililokuwa gumzo kubwa katika eneo hilo huku kila
mmoja akisema lake huku mmiliki wa nyumba hiyo kushindwa kuwa na majibu yakuridhisha
huku akisema yeye hafahamu shimo hilo limetokea wapi.
Handaki
hilo ambalo lilionwa na wachimbaji wa mitaro wa JR wanaoshuhulika na
uwekwaji wa mabomba mapya ya maji safi. Wachimbaji hao wa mitaro wanaeleza kuwa
wakati wanachimba walikutana na chemba hiyo ikiwa imefunikwa na wao kudhani
kuwa inatumika kama shimo la choo cha nje lakini haikuwa hivyo maana lilikuwa
wazi limejengewa na hakuna dalili ya kutumika kama choo.
Mmoja
wa wananchi aliyeingia katika handaki hilo Abdukareem ameeleza kuwa yeye ni
mkazi wa eneo hilo na alipopata taarifa alifika akiwa na mwenzake aliyefahamika
kwa jina la Salehe na kukubaliana kuingia ndani ili kufahamu kilichopo. Kutokana
na shimo hilo kuwa refu walitafuta ngazi lakini hawakufanikiwa kwani ngazi hiyo
ilikuwa pana na kuamua kutafuta fimbo kubwa ya muanzi na kamba na ndipo
walipofanikiwa kuingia ndani. Walipofika ndani walikuta chumba ambacho ni kama
futi tatu na kuona vidirisha vidogo kwa mbele huku bado kukiwa kumejengewa kwa
zege na kubainisha kuna muendelezo wa chemba nyingine ambapo hawakuweza
kuendelea kwakuwa kumezibwa.
Mkuu
wa wilaya ya Iringa Dkt Leticia Warioba alifika katika eneo la tukio akiwa na
wa wafanyakazi wa Kampuni ya JR pamoja na afisa usalama ambao waliishia
kuangalia njia hiyo pasipo kuingia ndani ya handaki hilo.
Wakazi
waliofika katika eneo hilo hawakusita kueleza hisia zao huku wengine wakieleza
labda ni mahandaki yaliyokuwa yakitumiwa na Wajerumani enzi za ukoloni, huku
wengine wakieleza labda handaki hilo limekuwa likitumiwa na majambazi kama
sehemu za kujificha na kuhifadhia mali walizoiba japo hapakuonekana mali ya aina
yeyote.
PICHA
NA FRANCIS GODWIN
No comments:
Post a Comment