Narudia
tena na tena na safari hii kwa kusisitiza: Mwaka 2015 sitagombea Ubunge, nitafanya
kampeni ya Urais, ama mimi kama mgombea wa chama changu CHADEMA au kama mpiga
debe wa mgombea wa chama changu. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo
ni vema niwaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa
wetu wa Kigoma. Huu ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa
Jimbo langu na mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005.
No comments:
Post a Comment