Basi la Kampuni ya Dar express linalofanya
safari zake kati Dar Es Salaam na Arusha limeteketea kwa mot oleo eneo la
Segera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga. Kwa mujibu wa habari zilizoifikia
Mwanatanga ni kwamba zahama hiyo ilitokea muda mfupi baada ya basi hilo
kusimama eneo hilo maarufu la Segera ambayo ni njia panda ya Tanga , Dar es
Salaam na Arusha.
Mbali na moto huo kuteketeza kabisa
basi hilo hakuna majeruhi wala aliyepoteza maisha kufuatia ajali hiyo
mbaya. Aidha mwanatanga inadhani ni
wakati muafaka sasa kwa wenye Mabasi pamoja na Mamlaka kuchukua tahadhari za
Kiukaguzi kabla ya mabasi hayo kuanza Safari ili kuweza kuepusha ajali ambazo
zinaweza kuepukika. Jumla ya abiria
wapatao 65 wamenusurika kufuatia ajali hiyo. Picha za tukio zima hizi hapa.
No comments:
Post a Comment