BM BARBERSHOP KINONDONI

Tuesday, April 9, 2013

MASHUJAA MUSICA YATOA RISASI KWA MCD-YASEMA ALIKUWA ANAWAKERA WENZAKE NA MASHABIKI KWA TABIA ZAKE


MCD akicharaza Tumba


BENDI ya muziki wa Dansi nchini Mashujaa imetanabahisha kuwa mwanamuzi wake MCD aliyerejea kwenye Bendi yake ya zamani Twanga Pepeta alikuwa akirudisha nyuma maendeleo ya Bendi hizo kutokana na sababu mbalimbali kama zifuatazo:
1.       Mpiga Tumba huyo alikuwa na tatizo la kutowaamini wenzake
2.       Alikuwa anapenda kupanga upya sauti kila anapopanda yeyé jukwaani kazi ambayo huifanya kwa zaidi ya saa nzima huku wapenzi wakisubiri muziki.
3.       Alikuwa na tabia ya kubomoa na kuvipanga upya vyombo hata kama wenzake walikuwa wakiendelea kutoa burudani
4.       Pamoja na nafasi kubwa aliyopewa kutokana na heshima na umri wake lakini bado alikuwa ni mchelewaji nambari moja kazini na kutoa sababu zisizotosheleza
Tabia hizi zilikuwa ni kero kwa wanamuziki wenzake pamoja na Washabiki kwa ujumla.
Chanzo cha habari hii ni. Gazeti la Dimba Jumatano Aprili 10-13 TOLEO NA. 2718

No comments:

Post a Comment