MWANAMKE huyu ambaye
hakufahamika jina lake amekutwa katika mazingira haya jana alfajiri maeneo ya
Ilomba Jijini Mbeya akiwa kama alivyozaliwa, Inadaiwa kuwa mwanamke huyu ni
mmoja wa wanafunzi wa chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU).
Wananchi walikusanyika katika
eneo alipokutwa mwanamama huyu ambapo inadaiwa kuwa alikuwa akiwanga nyakati za
usiku lakini akakutana na wababe wa Ulozi mitaa hiyo ndipo aliposhindwa kuendelea
na ulozi wake na kujikuta akikosa nguvu na kushindwa kuendelea na safari yake
ya ulozi hadi alipokutwa asubuhi kweupee!!!
Inaelezwa kuwa eneo hilo ni
maarufu kwa kukamata watu wanaoingia anga hizo kwa ajili ya kufanya ugagula
ambapo miezi michache iliyopita mtoto mdogo wa kike naye alibambwa akitaka
kufanya ulozi na kukutwa na umati wa watu kabla ya kufanya ulozi wake.
Mwanamke huyu aliokolewa na
askari polisi ambao walimchukua moja kwa moja hadi kituoni kwa ajili ya
kuhifadhiwa ili asipate madhara zaidi. Jitihada za kukutana na uongozi wa chuo
kikuu cha TEKU zinaendelea ili kujua kama mwanamke huyu alikuwa ni mwanafunzi
wa chuo hicho kama inavyoelezwa na watu ama la.
No comments:
Post a Comment