Binti
wa Kipare ambaye amewahi kuvuma miaka kadhaa iliyopita na kupamba vyombo vingi
vya habari hasa Magazeti ya UDAKU Christina Manongi 'Sintah' ambaye siku za
karibuni aliripotiwa kusambaza picha za UTUPU za mwanadada anayeibuikia kwenye
TASNIA ya uimbaji Agness Gerald Masogange. Sintah ni motto wa kwanza wa Mzee
John Manongi anayeishi Sinza mwenyeji wa KIHURIO mkoani Kilimanjaro Wilaya ya
Same. Muigizaji huyu aliyetengeneza jina kupitia kikundi cha Kaole Sanaa Group
amempiga mkwara mzito Masogange na kumuambia AFUNGE BAKULI LAKE kwani
akiendelea atatoa picha zake za UTUPU moja baada ya nyingine ili kumnyamazisha
Kabisa.
Sintah
ambaye alikulia eneo la KINONDONI SHAMBA kwa shangazi yake ajulikanaye kwa Jina
la Mama Shem aliongea na Mwanatanga kwenye Saloon ijulikanayo kama Twins Saloon
iliyoko Kinondoni Muslim mbele ya Dada yake aliyejitambulisha kwa jina la
Sakina Shem na kuapa kumdhalilisha zaidi binti huyo Masogange kama ataendelea
kumfuatafuata. Aidha muigizaji huyu mwenye mbwembwe nyingi
kutoka ndani ya tasnia ya filamu za Kibongo amemtaka video queen wa
Bongo Agness Gerald Masogange kuacha kumsingizia kwenye SAKATA hili
la picha za utupu kwakuwa yeye hahusiki.
Sintah
amesema kuwa amesikitishwa sana na kitendo cha Agness kumtaja yeye
(Sintah) kuwa ndiye anahusika na kuisambaza kwenye mitandao video
inayomuonyesha Agness akiwa mtupu huku pia akionekana kufanaya matendo
kadhaa ya kingono.
"Nimemsikia
na isitoshe kuna watu wengi wameniambia juu ya hilo la kunitukana na kunitaja
redioni kuwa nahusika, mimi sijui lolote awaulize marafiki zake
ambao mimi naamini ndiyo wanahusika kuzisambaza kwani hata kwenye BBM yangu ni
wao ndiyo walinitumia namuomba afunge bakuli lake la siivyo nitazitoa
zaidi kwani ninazo pati wani mpaka 3 na zote nimetumiwa na marafiki zake ambao
yeye anacheka nao lakini hajui kama ni ma-sn***ch" alisema Sintah.
Akiendelea
zaidi Sintah amefunguka kuwa kamwe hajui lolote kuhusu kamera anayoisema
Agnes, kwani binafasi hajawahi kukutana naye na alimjua
kupitia nyimbo za wasanii wa Bongo Fleva kwa kuwa msichana huyo
anapenda kuuza sura na zaidi hajui hata anapokaa.
Aidha
mwanatanga alimuuliza Sintah swali la kizushi kuhusu hali yake ya NDOA ambayo
ilifanyika miaka kadhaa nyuma kati yake na kijana wa Kiganda na send off Part
yake kufanyika pale Msasani Beach Club na kushuhudiwa na mamia ya marafiki zake
na baadaye Wedding mjini Kampala Uganda. Sintah alijibu kuwa hayo ni maisha
binafsi wala hayahusiani na mada inayozungumziwa. Swali hili la kizushi
lilikuja baada ya Tetesi kuwa anamahusiano ya Kimapenzi na Mchezaji wa Simba SC
Emmanuel Anthony Okwi. Katika hili alidai kuwa kwani kuna ubaya gani mimi kuwa
mahusiano na OKWI??? Kauli hii iliendelea kuacha tungo tata na mwanatanga
kuamua kuachana na hili kwakuwa lengo si kuingilia maisha ya mtu kwa undani.
No comments:
Post a Comment