ASILI
yake ni huko mkoani Tanga yalikozaliwa mapenzi!!! Kabila lake ni Mbondei au
wanabonde wa pale viwanja vya Muheza. Jina lake lilianza kukua kupitia
ulimwengu wa habari. Alikuwa mtangazaji baadaye akapita kwenye Shindano la
Kimwana Manywele Twanga Pepeta 2006/07 na sasa anafurukuta zaidi katika
ulimwengu wa filamu za Kibongo. Huyu si
mwingine bali ni Mwanadada Lulu Mathias Semagongo ‘Aunt Lulu’. Aliyezaliwa
mwaka 1987 jijini Dar es Salaam.
UTANGAZAJI
Kipaji kwa Aunt Lulu kilijionesha waziwazi tangu akiwa shule ya msingi. Mwaka 1998 hadi 2003 alikuwa akitangaza kipindi cha watoto cha Redio One na ITV kilichojulikana kwa jina la Watoto Show.
Mwaka 2004 hadi 2006, mkali huyo aliyeonyesha cheche katika kutumia kipaza sauti, alihamia Redio Magic FM ya jijini Dar. Akiwa Redio Magic Lulu alitangaza kipindi kilichofahamika kama Ulingo wa Watoto, wakati huohuo akiwa kwenye mtandao wa vijana uliokuwa ukijishughulisha na matatizo yanayowakabili watoto chini ya mfuko wa shirika linalojishughulisha na haki za watoto duniani la UNICEF.
LULU NDANI YA BENCH MARK PRODUCTION
LULU ARUDI DARASANI
Lulu
Mathais alianza shule ya msingi mwaka
1993 Shule ya Msingi ya Kumbukumbu iliyopo Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es
Salaam na kuhitimu elimu ya kuondoa ujinga kichwani mwaka 1999. Mwaka 2000, Aunt Lulu alijiunga na Shule ya
Sekondari Kisutu wasichana na kumaliza hapo mwaka 2004 kiwango cha elimu ya
Sekondari (O-Level).
UTANGAZAJI
Kipaji kwa Aunt Lulu kilijionesha waziwazi tangu akiwa shule ya msingi. Mwaka 1998 hadi 2003 alikuwa akitangaza kipindi cha watoto cha Redio One na ITV kilichojulikana kwa jina la Watoto Show.
Mwaka 2004 hadi 2006, mkali huyo aliyeonyesha cheche katika kutumia kipaza sauti, alihamia Redio Magic FM ya jijini Dar. Akiwa Redio Magic Lulu alitangaza kipindi kilichofahamika kama Ulingo wa Watoto, wakati huohuo akiwa kwenye mtandao wa vijana uliokuwa ukijishughulisha na matatizo yanayowakabili watoto chini ya mfuko wa shirika linalojishughulisha na haki za watoto duniani la UNICEF.
KIMWANA WA TWANGA PEPETA.
Mwenye
kipaji siku zote siyo mwenzako, mwaka 2006, Aunt Lulu alijitosa kwenye Shindano
la Kimwana wa Twanga Pepeta (Kimwana Manywele Twanga Pepeta) lililokuwa
likitafuta mnenguaji bora. Aunt Lulu alijishindia taji hilo na kunyakuwa zawadi
ya gari. Jina la Lulu lilianza kukua zaidi baada ya kupitia Kimwana Manywele. Aunt Lulu alitumia nafasi hiyo kusoma kozi
fupi za kompyuta kabla ya kujiunga na kampuni ya Bench Mark Production mwaka
2007.
LULU NDANI YA BENCH MARK PRODUCTION
Lulu
Mathias alijiunga na Kampuni ya Bench Mark Production kama Assistant Producer
na pia alikuwa host wa kipindi cha Wimbo kilichorushwa kupitia ITV,”
LULU ARUDI DARASANI
Mwaka
2008, mtangazaji Lulu alirudi darasani na kusoma kozi ya Kingereza pale British
Council na kufanikiwa kuhitimu masomo hayo katika ngazi ya cheti (advanced
certificate).
Maisha
ya Aunt Lulu yaliendelea kushamiri katika kazi ingawa pia aligubikwa na skendo
za hapa na pale kama ulevi wa kupindukia na mengine mengi yanayofanana na hayo.
Mara kakutwa amelewa klabu, mara kanaswa sehemu na mwanaume na mengineyo.
UTANGAZAJI TENA
UTANGAZAJI TENA
Mwaka
2009 hadi 2011, Aunt Lulu mwenye matukio kibao mjini, alipata nafasi ya
kutangaza katika Televisheni ya C2C. Aliposimama kutangaza mwaka 2011, aliamua
kuingia kwenye darasa lihusulo taaluma yake ya utangazaji. Akajiunga na Shule
ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) kilichopo Makumbusho jijini
Dar es Salaam kupata cheti.
Mwaka
huu 2012, Aunt Lulu amekuja kivingine baada ya kugundua ana kipaji cha
uigizaji. Kwa kukubali ushauri aliopewa na mpenzi wake (Bond Bin Salim),
akaanza kuigiza chini ya Kampuni ya Richard Dyle Bezuidenhout (Richard wa BBA).
Mpaka
leo, Aunt Lulu bado anafanya shughuli za U-MC katika sherehe mbalimbali huku
akiwa ameelekeza nguvu zake katika ulimwengu wa filamu za Kibongo.
MAFANIKIO YA LULU
MAFANIKIO YA LULU
Mwenyewe
anasema mafanikio makubwa zaidi ni kujulikana, ukiacha kiwanja chake
alichonunua ambacho bado hajaanza ujenzi.
HUYU NDIYE LULU
MATHIAS MAGONGO “AUNT LULU”
na kweli ni lulu kweli mdau wangu karibu knjaro
ReplyDelete