Bendi ya Mashujaa Musica imemtambulisha mcheza shoo Super K ambaye alikuwa
Umangani akicheza shoo baada ya kuwa nje ya ULINGO wa Twanga Pepeta kwa miaezi
Sita akiwa huko Uarabuni akicheza Shoo kwenye kumbi za Hoteli. Ushawishi wa
Super K kuhamia Mashujaa ulifanywa na Rais wa Bend hiyo Charles Gabriel Mbwana
(Torres) ambaye alikutana na Super K Dubai alipokwenda miezi zaidi ya minne
iliyopita wakati akiwa safarini kuhamia Mashujaa Band.
Uongozi wa ASET ulilitambua hili tangu wakati huo na Super K aliongea na
mwanatanga kuhusu kuhamia kwake Mashujaa kwa Dau ambalo ni pesa aliyokabidhiwa
siku alipotua Airport akitokea Uarabuni wiki kadhaa zilizopita. Aidha Super K
alifika kwenye Mazoezi ya bendi ya Twanga Pepeta siku ya Jumanne na kukuta
mazoezi yakiendelea huku kukiwa na Wacheza shoo LUKUKI ambao watatambulishwa
PUNDE baada ya Ramadhani. Super K aliambiwa na Asha Baraka kuwa RUKSA kwenda
unakotaka ili ukatafute maisha sisi tupo na tunaendelea KUJIKONGOJA. Kauli hii
ilimfanya Super K atabasabu na kukana kutojiunga na Mashujaa lakini kila
Mwanamuziki aliyekuwepo siku hiyo ya mazoezi alibariki safari ya mcheza Shoo
huyu na kusema kuwa Twanga Sera zake sasa nikuwa na Safu ya Wacheza Shoo wa
Kike na ndiyo maana haijaongeza Mcheza shoo wa kiume hata mmoja tangu kuondoka
kwa kina Nyamwela, Danger Boy na sasa yeye Supr K.
"Uwanja uko wazi kwa yoyote anayeona anataka
kwenda kutafuta maslahi kwakuwa Twanga haina Fedha chafu" alisema Mama
Asha Baraka. Wiki hii imeripotiwa kuwa Mcheza Shoo Lilian Internet na Mpiga
Gitaa Ally Akida waliokuwa Twanga Pepeta na kuhamia Mashujaa wameachana na
Bendi hiyo na kuamua kurejea Twanga Pepeta. Uongozi wa Mashujaa na Twanga
pepeta uliulizwa na yafuatayo ni Mahojiano juu ya Jambo hilo.
Mwanatanga
ilijaribu kumtafuta Ally Akida na kumuuliza kama ifutavyo – Mzee wa Bunju vipi
mbona nasikia huonekani kazini takribani Mwezi sasa kwenye Bendi yako ya
Mashujaa???
Majibu ya Ally Akida- Kaka nimeamua kuachana na bendi ya Mashujaa Musica
kwasababu hawana roho ya huruma mimi nilikuwa namuuguza mwanangu viongozi wote
walikuwa na taarifa nashangaa wamenikata kiasi cha shilingi elfu sitini
(60,000) kwenye mshahara wangu si utapeli huu bora nikae nyumbani nifanye mambo
yangu binafsi.
Swali kwa
Mashujaa Musica- Uvumi wa Ally Akida kuikacha Bendi yako kwa madai ya kukatwa
pesa yake ya mshahara una ukweli ndani yake???
Mashujaa Musica -
Kuhusu Ally Akida ni kweli hayuko
kazini mwezi sasa,hata ivyo suala lake bado liko ofisini na hajaacha kazi rasmi
kwani ana vitu vya kukabidhi kama ni kweli, Na kuhusu Liliani ni uvumi huo
labda unatokana na yeye kuomba likizo ya Ramadhani huo ni uzushi. Ndiyo maana
nina uhakika ni uzushi na kuhusu Ally Akida hajatoa taarifa rasmi hivyo bado ni
mfanyakazi mpaka hapo atakapoandika rasmi barua ya kuacha kwani ana mkataba,
hata hivyo tuko tayari kumuachia kama akitamka rasmi na si kupitia katika
magazeti;DEO unajua strategically ilikuwa lazima kuboost jina through big names
lakini trust me mipango ya baadae ya bendi ni jina la bendi kwanza na through the
reputed name we can nurture the young talented...
Swali kwa ASET- Ni kweli Ally Akida anataka kurejea Twanga Pepeta, na vipi
kuhusu Lilian Internet kuwepo kwenye Mazoezi ya Twanga Pepeta???
Jibu kutoka ASET- Kaka Deo Twanga ni Bendi kubwa watu wanatoka na wengine
wanaingia na wale wanaotoka baadaye hurejea hivyo hilo si jambo geni kwenye
Bendi hii Kongwe.
Majibu haya yalinipa
Picha ya kutaka kujua kitakachofuata… Twanga wameahidi kuendelea kufanya kazi
na kutaka niwe na subira hadi mwezi MTUKUFU uishe.
No comments:
Post a Comment