Taarifa
ambayo imewashtua watu wengi inamuhusu mwanamama Valerie Spruill ambae ameishi
na baba yake mzazi kama mke na mume kwa miaka 40 bila kugundua. kwa mujibu wa
Daily Post Nigeria, Spruill aligundua hii siri mwaka 2004 na amewavutia wengi
kwa ujasiri wake wa kuiweka wazi kuhusu mumewe ambae kwa sasa ni marehemu.
Chanzo
cha yeye kufahamu ni kutokana na kukusanya taarifa mbalimbali ambazo mwanzoni
alianza kuzipata kama tetesi za umbea kutoka kwa watu mbalimbali. Mpaka sasa
mama huyu mwenye umri wa miaka 60 ana watoto watatu na wajukuu nane na
alifahamu ukweli wa hii ishu kupitia kwa Uncle wake siku chache baada ya kifo
cha mume wake. Umeshawahi
kusikia kisa cha aina hii? unemfahamu yeyote? mawazo yako ni yapi ili kuepuka
vitu kama hivi? share na mimi kwa kucomment mtu wangu wa nguvu.
No comments:
Post a Comment