BM BARBERSHOP KINONDONI

Thursday, October 25, 2012

VIONGOZI WA UAMSHO WARUDISHWA RUMANDE TENA

Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Sheikh Farid Hadi Ahmed kushoto akiwa na wenzake sita walioletwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga wakiwa hawana ndevu na kufunguliwa mashtaka manne mapya mahakamani hapo yakiwemo kuharibu mali za watu zenye thamani ya Shl.Milioni 50 na kufanya vurugu za makusudi zakuhatarisha amani katika nchi…Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
Mawakili wa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Abdallah Juma kushoto na Salim Tawfik wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu kujitoa kwao siku ya leo katika kesi hiyo kutokana na usmbufu wanaofanyiwa wateja wao wa kuhawangaishwa na kukosa kupelekwa Mahakama ya Kwerekwe kwa muda muafa..Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

Baadhi ya Askari wa kutuliza fujo wakiwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga kwa lengo la kutuliza amani Mahakamani hapo.. Picha na MakameMshenga-Maelezo Zanzibar

Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO wakiwa wanatoka katika Mahakama Kuu ya Zanzibar Vuga baada ya kufunguliwa mashtaka manne mapya..Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

1 comment:

  1. Hao uamsho lazima watambue kama zanzibar kuna utawala wa sheria. Wanachotaka kufanya uamsho hakina tofauti na kile kichofanywa na al Shabaab Somalia. Kutia hisia kali za kidini kwa wafuasi wao ili watwae dola bila idhini ya wananchi. Wazanzibari wasipokua macho watarejeshwa 1963 kwenye sultani wa kiarabu. Nadhani sicho wanachokitaka wazanzibari walio wengi.

    ReplyDelete