Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Rais wa Baraza la Maaskofu
Katoliki Tanzania, Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa kufuatia kifo
cha Askofu wa Kwanza wa Jimbo Katoliki la Mpanda, Baba Askofu William Pascal
Kikoti.
Kifo cha Askofu Kikoti kilitokea jana Jumanne tarehe 28 Agosti, 2012 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mkoani Mwanza alikokuwa amelazwa kwa matibabu kutokana na ugonjwa wa Shinikizo la Damu.
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na
taarifa za kifo cha Baba Askofu William Pascal Kikoti wa Jimbo Katoliki la Mpanda
akiwa bado na umri mdogo wa miaka 55 wakati ndiyo kwanza utumishi wake ulikuwa
ukihitajika zaidi, Ni dhahiri kwamba kifo cha Baba Askofu Kikoti kimeacha pengo
kubwa la kiuongozi siyo tu kwa Kanisa Katoliki hapa nchini, bali pia Jumuiya ya
Waamini wa Kanisa hilo kote duniani ninatambua jitihada kubwa za Marehemu Baba
Askofu William Pascal Kikoti enzi za uhai wake katika kuwatumikia Waumini wa Kanisa
lake, na hususan wa Jimbo Katoliki la Mpanda, tangu alipopata Daraja la Upadre
mwaka 1988, kuteuliwa kwake kuwa Askofu wa Kwanza waJimbo Katoliki la Mpanda
mwaka 2000, na hatimaye alipowekwa Wakfu na Kusimikwa kuwa Askofu wa Jimbo hilo
mwaka 2001. Kutokana na msiba huo mkubwa, ninakutumia wewe Baba Askofu
Tarcisius
Ngalalekumtwa, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Salamu zangu za Rambirambi, na kupitia kwako kwa Kanisa Katoliki na kwa Waumini wote
wa Kanisa hilo hapa nchini hususan wa Jimbo Katoliki la Mpanda, kwa kumpoteza mmoja wa Viongozi muhimu na wa ngazi ya juu wa kiroho, Marehemu Baba Askofu William Pascal Kikoti. Ninamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipumzishe mahala pema peponi Roho ya Marehemu. Ninawahakikishia wote waliofikwa na msiba huo kuwa niko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo kwakutambua kuwa yote ni mapenzi yake Mola.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
29 Agosti, 2012
No comments:
Post a Comment