JARIDA
maarufu la Times nchini Uganda limemtaja mama wa watoto
wawili Zari Hassan kuwa ndiye mwanamke mrembo na tajiri kuliko wote nchini humo
kwa wakati huu.
Kwa
mujibu wa Jarida hilo Zari mwenye umri wa miaka (30) ambaye ni
Mwanamuziki, Mfanyabiashara na Mtangazaji wa runinga amepata
mafanikio makubwa kwenye muziki na pia kipindi chake cha
runinga kinachofananishwa na kipindi cha ‘Keeping up with the
Kardashians’ kinachoendeshwa na mrimbwende wa kimarekani Kim Kardashian.
Huku likiambatanisha picha
za magari na nyumba anazomiliki mwanadada huyo, jarida hilo
limeandika kuwa huenda akaingia kwenye orodha ya wanawake matajiri
zaidi Afrika baada ya kipindi kifupi kijacho endapo ataendelea na mwenendo wake
wa sasa kibiashara. Hata hivyo jarida hilo pia limemtaja Zari
kuwa mmoja wa Mastaa wapenda starehe na amekuwa akitumia
mkwanja alionao kumnasa mwanaume wa aina yoyote anayehisi kuwa
anahitaji kumliwaza kwa wakati huo ingawa tuhuma hizo hazikuthibitishwa moja
kwa moja.
Katika hatua
nyingine Jarida hilo limesema kuwa Zari mwenye maskani yake pia
nchini Afrika ya Kusini, wazazi wake si raia wa Uganda kwa kuzaliwa isipokuwa
ni wahamiaji kwani baba yake ni raia wa Burundi mwenye asili ya Somalia
na mama yake ni raia wa India kutoka kabila la Mutoroo.
Aidha Times limeatanabahisha
kuwa Zari anamiliki ndinga kibao za kisasa na zenye thamani kubwa kama
BMW – 2006, Black Chrysler – 2008, – Audi Q7 2010 Silver Crysler – 2008,
JETTA-2006, Mercedes Benz convertible -2008. Range-Rover, Lamborghin, Hummer
na mengine mengi huku pia akiwa na umiliki wa maduka, Hoteli na
majumba ya kisasa kwenye miji mikubwa ya Pretoria, Cape Town na Kampala.
No comments:
Post a Comment