BM BARBERSHOP KINONDONI

Tuesday, August 21, 2012

MRATIBU WA ELIMU AMBAYE PIA NI SHEIKH MBARONI KWA KUHAMASISHA WANANCHI KUSUSIA ZOEZI LA SENSA




Wakati siku zikikaribia za kufanyika zoezi la Sensa ya watu na makazi, Mratibu mmoja wa Elimu Kata ya Vugiri wilayani Korogwe, Tanga, Juma Salehe (52) amekamatwa na polisi akihamasisha mitaani kwa kipaza sauti wananchi walikatae zoezi hilo.

Habari zilizofikia Mwanatanga Blog ambaye anatokea Wilaya na Korogwe Mjini,  zimesema mratibu huyo wa elimu ambaye anadaiwa kuwa Sheikhe wa Msikiti wa Mazinde katika kata hiyo ya Vugiri anashikiliwa katika kituo cha mamlaka mji mdogo wa Mombo uliopo wilaya ya Korogwe vijijini mkaoni Tanga.

Imeelezwa amekamatwa jana saa 8.00 mchana ndani ya msikiti wa Mazinde, kutokana na  wananchi kutoa taarifa dhidi ya mtu huyo kuendesha vitendo ambavyo vilikuwa vikiwachanganya wananchi kuhusu zoezi hilo la Sensa.

"Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa maandalizi ya shitaka lake", amesema Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,Coastantin Massawe.

No comments:

Post a Comment