WAKATI
mfungaji bora wa klabu bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati ‘Kombe la
Kagame’ Yanga SC, Said Bahanuzi ‘Spider Man’ akitua nchini Rwanda leo,
mabingwa hao kesho watashuka katika Uwanja wa Nyamirambo Kigali, Rwanda
kuikabili Polisi ya huko katika mchezo wa kujipima nguvu.
Bahanuzi
hakuwemo katika msafara wa Yanga uliokwenda nchini Rwanda katikati ya wiki
iuliyopita kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Paul Kagame kwa ajili ya
kuwapongeza kutokana na kutwaa ubingwa wa Kagame iyoutwaa kwa mara ya pili
mfululizo wiki mbili zilizopita, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa kuifunga
Azam FC mabao 2-0, kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.
Bahanuzi
aliwasili huko kutokea Dar es Salaam na kuungana na wenzake ambapo kama kocha
ataridhika na kiwango chake huenda leo akacheza mechi yao dhidi ya
maafande.
Alisema
timu yao ambayo jana ilianza vema mechi zake za kujipima nguvu nchini humo
baada ya kuichapa Rayon Sport mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Amahoro mjini Kigali,
pamoja na ushindi huo ilipoteza mabao mengi ya wazi baada ya washambuliaji wake
kushindwa kutumia vema nafasi za wazi walizotengeneza.
mchezo
wa kesho na Polisi, unatrajiwa kuwa wa ushindani kwakuwa Mbelgiji Tom Saintfiet
alifanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza juzi hivyo anaamini kitashuka kikosi
bora zaidi. Mchezo wa leo utahitimisha ziara yao huko iliyoanza katikati
ya wiki iliyopita abapo keshokutwa wanatarajiwa kurejea jijini Dar es
Salaam keshokutwa kuendelea na maandalizi mengine ya ligi kuu soka Tanzania
Bara inayotarajiwa kuanza Septemba 15.
Pamoja
na michezo hiyo, Yanga ilipata kuzuru makumbusho ya Kimbari ambayo walizikwa
wahanga waliofariki katika mauaji yaliyotokea nchini humo mwaka 1994 kutokana
na ugombi wa kikabila.
Yanga
pia ilipata fursa ya kutembea Ikulu ya Rwanda na kuonana na Rais Kagame ambapo
walizungumza maswala mbalimbali ikiwemo mikakati ya kuendeleza uhusiano mzuri
wa kimichezo baina yao.
No comments:
Post a Comment