MIRINDA NYEUSI NA KALALA JUNIOR |
Bendi ya African Stars Twanga Pepeta itafanya ziara
kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini itakayohusisha Mikoa ya Iringa na Mbeya
kuanzia siku ya Ijumaa tarehe 14/09/2012 kwa siku tatu Mfululizo. Ziara hiyo ni
kutokana na ahadi ambayo ilishawekwa hadharani mapema wakati Mwanamuziki Kalala
Junior anarejea Twanga Pepeta kutoka Bendi ya Mapacha 3.
KIONGOZI WA BENDI LUIZER MBUTU |
Ziara
hiyo itaanza kwa onyesho maalum ndani ya Ukumbi wa Highland uliopo
mjini Irnga kwa ajili mya kuwaonyesha wakazi wa mji wenye Vilima vyenye
mawe vya Kihesa, Ilala, Ndiuka, Mwembetogwa na baadhi ya maeneo maarufu kwenye
mji huo wenye hali ya baridi unaosifiwa kuwa wa pili kwa Usafi baada ya Moshi. Kwa
mujibu wa Meneja wa ASET Muddy K taratibu za ziara hiyo maalum zimekamilika.
Onyesho
la pili linatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi 15/09/2012 Jijini Mbeya ndani
ya City Pub na kesho yake yaani siku ya Jumapili tarehe 16-09-2012 kumalizia
kwa kufanya Bonanza maalum katika ukumbi huo huo wa City Pub kufuatia ombi
maalum katika kuhitimisha ziara hiyo inayojulikana kama Amsha Amsha na Twanga
NYANDA ZA JUU KUSINI.
Bendi
ya Twanga Pepeta inatarajia kuondoka alfajiri ya tarehe 14/09/2012 siku ya
Ijumaa baada ya Onyesho la Club Maisha Oysterbay. Bendi inataraji kurejea Dar
Es Salaam baada ya onyesho la mwisho litakalofanyika siku Jumapili tarehe
16-09-2012 Jijini Mbeya.
MARY KIMWANA ZAO LA TWANGA PEPETA |
Ziara
hii maalum ya Twanga Pepeta ni kwa ajili ya kumtambulisha Mwimbaji wao mpya
Kalala Jr aliyerejea hivi karibuni kutoka katika Bendi ya Mapacha Watatu ambayo pia itatumika
kuzitambulisha nyimbo mpya za bendi kwa mwaka 2012 ammbazo ni pamoja na; Shamba
la Twanga (Greyson Semsekwa, Mapambano ya Kipato (Prince Mwinjuma Muumini, Walimwengu
(Jumanne Said), Nyumbani ni Nyumbani (Kalala Jr) na Ngumu Kumeza (Mirinda
Nyeusi). Twanga Pepeta itaendelea na Burudani zake kama kawaida Jijini Dar es
salaam katika kumbi za Club Billicanas siku ya Jumatano, New Club Maisha siku
ya Alhamisi, Free Time Resort Ukonga Banana, Mango Garden siku ya Jumamosi na
Jumapili mchana Leaders Club na usiku Mzalendo Pub.
Wiki
inayofuata Twanga Pepeta itaendelea na Ziara kwenye Mikoa ya Kanda ya Ziwa
nakurejea Dar es Salaam na Baadaye Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kati, Kanda ya
Kusini na kumalizia na Visiwa vya Zanzibar vyenye Marashi ya Karafuu.
MUDDY K
EVENTS MANAGER
TWANGA PEPETA.
No comments:
Post a Comment