Unakumbuka
ni siku kadhaa zimepita toka kuandikwa kwa stori kubwa kwenye kiwanda cha
bongofleva kuhusu T.I.D kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kutaka kumuua
msanii mwenzake ambae ni Ally Kiba?
Baada ya
hiyo stori kutoka, kilipita kipindi kifupi cha ukimya lakini sasa hivi T.I.D
ameongea kwa upana zaidi kuhuu hizo tuhuma ambazo zilimfanya ashikiliwe na
polisi kwa mahojiano.
Kwenye
255 ya XXL Clouds Fm namnukuu akisema “hii kesi nashindwa kuielewa, mimi ni mtu
mzima sana alafu ukiniambia nina matatizo na Ally Kiba na wakati hata
sijagombana nae, hivi vitu hivi mtu unaenda kwa mganga unataka kujibust afu
mganga anakwambia bwana T.I.D ujue katoa ngoma kali anataka kukuua we
unachukulia serious, hivi vitu ni vya kijinga sana unatakiwa kufikiria”
Kwenye
sentesi ya pili, T.I.D amesema “Polisi wamechukua pin namba yangu, sim namba
yangu na kwenda kufanya uchunguzi hakuna connection yoyote ya mimi kwamba
nimeongea na Ally Kiba au nimeongea na mtu yeyote ambae anataka kumuua Ally
Kiba kwa hiyo ni uongo, sasa mimi kwa fikra yangu kama mtu mzima nafikiria huyu
kijana huyu, mganga ambae amemshauri yeye ajibust kupitia section hiyo,
amekoseaaa amekosea sana kwa sababu tunaamini kwenye kipaji”
Sentensi
ya tatu ya maneno ya T.I.D ni “yeye kama anataka kuwa mkali kunizidi mimi
ajifue atoe ngoma kali lakini hakuna mtu anaemchukia, mimi nampenda sana na
kama yeye anakataa mimi simpendi kwa nini ameingia kwenye remix yangu na
nimemuweka pale, remix nilitaka niitoe sema walivyoniweka ngome kidogo nimejisikia
kama wananichukia, lakini mimi nitaitoa hii ngoma na mimi sijibust kama
wanavyojibust na hawaniwezi”
Sentensi
ya nne ya kauli ya Top in Dar ni “wanataka kuniweka ndani, wanataka kunifunga
jela lakini mi naomba kabla hawajaniweka ndani niwape show hii apa ya usiku wa
viuno sunday hapa kesho kutwa Bills, nitakua mimi na wakali wote Ngwea, Profesa
Jay kwa sababu tunazindua ile single mpya ya ‘raha’ alafu kona lake”
Kuhusu
kesi, namnukuu T.I.D akisema “kesi lazima iende kwa mwanasheria
mkuu kuangalia kama inaweza kuwa kesi lakini imerudishwa imeonekana haiwezi
kuwa kesi kwa sababu haina ushahidi wowote, inaonekana tu vitu vya imagination
ambavyo mtu kapanga vifanyike lakini kwa sababu wao wanaendelea kutaka kesi na
mimi nataka wao pia niwafungulie kesi kwa kunidhalilisha”Ukitaka
ushahidi wa kumsikia T.I.D mwenyewe, bonyeza play hapo chini…
No comments:
Post a Comment